ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 13, 2017

WACANADA WAANDAMANA KUPINGA ZIARA YA FAMILIA YA TRUMP KATIKA MJI WA VANCOUVER.

Wakazi wa mji wa Vancouver, Canada wamefanya maandamano makubwa kupinga ziara ya familia ya Rais Donald Trump wa Marekani katika mji huo.
Maandamano hayo yamefanyika baada ya baadhi ya watu wa familia ya Rais Trump, kuwasili mjini Vancouver kwa minajili ya kufungua hoteli mpya iliyopewa jina la 'Trump' na kulaani vikali ujio wa watu wa familia ya rais huyo anayepingwa kila kona ya dunia. Gazeti la Washington Post limeandika kuwa, katika ufunguzi wa hoteli hiyo, walifika watoto wawili wa kiume na binti ya rais huyo wa Marekani mjini hapo Vancouver.
Vijana wawili na mabinti wa Rais Donald Trump.
Gazeti hilo limewataja watoto hao kuwa ni 'Eric Trump' na 'Donald Trump Jr' watoto wawili wa kiume wa Trump na 'Tiffany Trump' binti mwingine wa Trump na kwamba watoto hao waliambatana na wake na waume zao chini ya ulinzi mkali. 

Baada ya kujulikana ujio wa watu wa familia ya rais huyo, wakazi wa Vancouver walikusanyika kwa wingi na kufanya maandamano ambayo yaliishia mbele ya jengo la hoteli waliyoenda kuifungua huku wakitoa nara zinazosema 'Watu wa Trump waondoke nchini kwetu.'  Baada ya Rais Trump kuingia madarakani nchini Marekani watoto wake ndio waliochukua jukumu la kupanua harakati za kiuchumi za familia ya Trump huku wakifanya safari katika nchi mbalimbali za dunia zikiwemo Uruguay, Ireland na Imarati.
Sehemu ya jumbe za maandamano hayo.
Hata hivyo kwa kawaida harakati hizo za kiuchumi zimekuwa zikipingwa vikali hata ndani ya Marekani kwenyewe. Wapinzani wanasema kuwa, harakati hizo zinatia wasi wasi mkubwa kutokana na utumiaji mbaya wa madaraka wa Rais Donald Trump na watu wake wa karibu ambapo anapanua wigo wake wa kiuchumi kupitia madaraka ya kisiasa aliyonayo hivi sasa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.