Hatua ya mkuu wa Mkoa John Mongela inafuatia ziara yake aliyoifanya kiwandani hapo tarehe 10 Julai, 2017 na kuwaamuru wahusika kuwa na mpango kazi ambao ungeonesha kwa namna gani wataanza kazi ifikapo Januari, 2018, huku akiwataka wahusika wote ambao wanamaslahi na kiwanda hicho kuwepo kiwandani hapo ifikapo 20 Julai, 2017.
Kinyume na matarajio ya Mkuu wa Mkoa, alipowasili kiwandani akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, majira ya saa 5.43 za asubuhi siku ya tarehe 20 Julai, 2017, alikuta hakuna maendeleo yoyote juu ya hatma ya kiwanda hicho na hata mpango kazi aliokuwa ameagiza hakuuona.
Akitoa maelezo mbele ya mkuu wa mkoa, Mwanasheria kutoka Kampuni ya Galati ya jiji Mwanza, Pendo Gimeno, alisema yeye anachofahamu wapo katika mchakato wa kuhamisha umiliki kutoka kwa mmiliki wa awali ambaye ni Casco kwenda kwa Sky Scraper zoezi ambali lilianza kwa makubaliano tokea mwaka 2015 lakini makabidhiano ya Jalada katika ofisi zao walilipata mwaka 2016.
Mkuu wa mkoa alipotaka kufahamu zaidi juu ya hatua walizofikia, mwanasheria huyo alionesha kutofahamu jambo lingene zaidi ya suala la uhamisho na hivyo kuzidi kuongeza sintofahamu ya jambo hilo.
Naye afisa wa Usalama wa kanda wa Kampuni ya Caspian, Nurdin Suleiman, ambao wanaingia katika kadhia hiyo, kufatia kugeuza eneo la kiwanda hicho kuwa sehemu ya kutunzia baadhi ya mitambo yao, alipohojiwa ni lini wataondoa vifaa vyao ilikupisha shughuli zilizo kusudiwa kuendelea, alisema wao wapo tayari kuviondoa vifaa vyao lakini kufuatia utata uliopo ndio maana wameshindwa kuviondoa, huku akitaja kupata hasara ya mali hizo.
“Mhe. Mkuu wa Mkoa sisi tupo tayari kuondosha mali zetu hata sasa, lakini vikwazo ambavyo tumevipata ni kuwa vitu vyetu vimengiwa sio chini ya miaka miwili, lakini tuliitika wito wa Mh. Mkuu wa mkoa na tulikuwa tayari kuondoa lakini Quality Group ndio walituzuia kuondosha” alisema Nurdin.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa, akaomba ushauri kutoka kwa baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama aliokuwa ameambatana nao akiwapo Katibu Tawala wa Mkoa, ambaye katika ushauri alioutoa, ilikuwa nikutafutwa kwa mmiliki hadi hapo atakapo patikana, ili hali Captain wa Jeshi la wananchi la Tanzania, akimashauri mkuu wa mkoa kuliweka eneo hilo chini ya uangalizi wa serikali hadi hapo sintofahamu iliyopo itakapo malizika.
Kufuatia ushauri alioupata, ndipo hapo mkuu wa mkoa akaamuru kufungwa kwaKiwanda hicho na kisha funguo kuwa chini ya ofisi ya mkuu wa mkoa hadi hapo suluhu itakapo patikana, “Kwamba kuna kamgogoro hapa, serikali ilibinafsisha viwanda hiki ili kiendelezwe katika sekta hiyo hiyo ya ngozi na hata Mhe. Rais mara nyingi amesema juu ya viwanda hivi juu yakuvifufua, aliema Mongella na kuongeza, kwamba alipofika tarehe 10 Julai, 2017 ilikuwa kutoa maelekezo juu kuondoshe vifaa vyote.
Mongella alisema, kwakuwa shughuli hiyo niya kitaalam nilazima sekta zote zihusishwe ikiwapo watu wa Wizara ya Viwanda, watu wa ubinafsishaji na watu wa ardhi lazima wawe pamoja “Kwa sasa Jengo hili litakuwa chini ya Ofisi yangu na funguo tunaondoka nazo na hakuna mtu mwingine, nakwa uapande wa wale waliopanga kama Caspian na Vodacom wasubiri lakini waendelee na biashara zao” alihitimisha, huku akimtaka Katibu Tawala wa Mkoa kuweka ulinzi katika eneo hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.