Akizungumza na Blogu hii, mwanzilishi wa kampuni hiyo Mwesiga Kyaruzi amesema kwamba kutokana na mahitaji ya soko la habari, mawasiliano na masoko ambapo watu wengi hivi sasa wanategemea zaidi kupata habari haraka zaidi kupitia mitandao ya kijamii, kampuni yake imeona ni vyema kufungua akaunti ya Instagram ili kupanua wigo wa usambazaji habari za bidhaa na huduma zitolewazo na makampuni pamoja na taasisi mbalimbali zinazohudumiwa na kampuni hiyo.
“Pamoja na kuwafikia watu wengi zaidi wanaotumia huduma na bidhaa mbalimbali zitolewazo na wateja wetu, pia hii ni hatua thabiti ya kwenda na mahitaji ya wakati uliopo kwani takwimu zinaonyesha kwamba mtandao huo hadi kufikia mwezi April mwaka huu ulikuwa unatumiwa na watu wapatao milioni 800 kuzungumza na kupashana habari kwa mwezi, hivyo basi kwa mazingira ya dunia ya sasa ni muhimu kwenda na wakati badala ya kutegemea vyombo vya habari vya asili (traditional media) pekee kama magazeti, redio na TV kwani dunia inabadilika kwa kasi,” alisema Kyaruzi.
Kampuni ya Proaktiv Communications inatoa huduma za kujenga taswira kwa kuratibu utoaji habari chanya kuhusu matukio, bidhaa, huduma na masuala mbalimbali kwa sekta za kibenki, kilimo, madini, mawasiliano, usafirishaji, elimu, afya, ujenzi, viwanda, nishati, huduma za kifedha, burudani, michezo pamoja na utalii.
Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea tovuti ya kampuni hiyo www.proaktiv.co.tz na hakikisha unafollow akaunti ya Instagram kupitia link ya www.instagram.com/proaktivpr ili kujionea matukio na habari kemkem zinazoratibiwa na kampuni hiyo ya Kizalendo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.