Saif al-Islam Gaddafi, mwana wa pili wa aliyekuwa kiongozi wa Libya
Muammar Gaddafi anadaiwa kuwa huru baada ya kuzuiliwa kwa kipindi cha
miaka sita.
Kuna wasiwasi huenda hatua hiyo ikatikisa zaidi hali ya kisiasa na kiusalama nchini Libya.
Saif al-Islam anadaiwa kuachiliwa huru baada ya kupewa msamaha.
Ndiye aliyependelewa na babake kuwa mrithi wake na amekuwa akizuiliwa na
kundi la wanamgambo katika mji wa Zintan kwa miaka sita.
Wanamgambo hao wa Abu Bakr al-Siddiq Battalion walisema aliachiliwa huru Ijumaa lakini bado hajaoneshwa hadharani.
Taarifa nchini Libya zinasema kwa sasa yupo katika mji wa Bayda, mashariki mwa Libya, kwa jamaa zake.
Alikuwa amehukumiwa kifo na mahakama mjini Tripoli, magharibi mwa nchi hiyo bila yeye kufikishwa mahakamani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.