Yamkini watu wawili wamejeruhiwa, katika kile mashuhuda wanasema kuwa kisa cha umiminunaji wa risasi katika jimbo la Virginia mapema leo Jumatano.
Seneta wa Republican, Rand Paul, anasema kuwa alisikia mlio wa risasi ya kwanza, kisha ikafuatiwa na milio ya risasi.
Walinda usalama walijibu mashambulio hayo.
Bwana Scalise ambaye ni mwanachama wa chama cha Republican, anasemekana
alipigwa risasi kwenye makalio, huku ikisemekana kuwa afya yake haimo
hatarini kwani amefikishwa hospitalini kwa matibabu pamoja na walinzi
wake ambao pia walijeruhiwa na mshambuliaji.Idara ya Polisi huko Virginia, inasema kuwa imemtia mbaroni mshambuliaji.
Rais Donald Trump amesema kuwa: "Tumetamaushwa mno na janga hilo."
Katibu wa mawasiliano wa Ikulu ya White House , Sean Spicerameandika katika mtandao wa kijamii wa tweeter kuwa Rais Donald Trump anajulishwa kuhusiana na shambulio hilo.
Tupe maoni yako

0 comments:
Post a Comment