Mzee anusurika kufa akipambana na fisi aliyevamia zizi la mbuzi Kishapu. |
WATU wawili wa kijiji cha Nyashana Kata ya Kalebezo
Wilayani Sengerema wameuwawa na wengine
watano kujeruhiwa baada ya kuvamiwa na kushambuliwa na Fisi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Ahmed
Msangi amesema tukio hilo limetokea May
mosi saa 3 asubuhi na kuwataja Watu hao kuwa
ni Lucia Sinza (65) mkazi wa Kalebezo na mtoto mdogo Juma Amos (3) wakati wakiwa
shambani alitokea Fisi aliyewavamia na kupelekea kupoteza maisha yao.
Kamanda msangi amesema kuwa wakati mnyama huyo akiendelea kumshambulia marehemu Lucia, mtoto
wake aitwaye Kefreni Faida ( umri wake
haukufahamia mara moja)ambaye pia alikuwepo shambani hapo alikwenda kumsaidia mama yake, ndipo Fisi
alimuacha mama huyo kisha alimrukia Kefrida na kwamba kwa bahati mbaya alimng’ata mtoto
aliyekuwa amebebwa mgongoni (Juma Amosi)
na kupelekea jeraha kubwa lililosababisha kupoteza maisha.
“ kutokana na kusikia kelele silizokuwa zikitokea maeneo
hayo Watu na majirani walifika
eneo la tukio kwa ajili ya kutoa
msaada lakini pia baadhi yao
walijeruhiwa katika sehemu mbalimbali za
miili yao” amesema Msangi
Majeruhi hao ni sostenes
kisumu( 25), alijeruhiwa mkono wa kulia na paji la uso,Tekla lunilija (60), ambaye alijeruhiwa mkono wa kulia, Abeli
Wiliam (35), alijeruhiwa mguu wa kushoto pamoja na Musa Nyuma (40),
aliyejeruhiwa kisha kutolewa kiganja chote cha mkono wa kulia.
Kamanda Msangi amesema
askari walifika eneo la tukio na kushirikiana na wananchi na kisha kufanya
msako mkali wa kumtafuta fisi huyo na hatimaye kufanikiwa kumuuwa na kwamba majeruhi
hao wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya wilaya ya Sengerema na hali zao
zinaendelea vizuri.
Miili ya marehemu
tayali imefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu zao kwaajili ya mazishi
na Kamanda wa Polisi mkoani hapa na
Naibu kamishina wa Polisi Ahmed Msangi ametoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki
waliopatwa na msiba huo, huku akiwaomba wananchi kuwa makini pindi wanapokuwa
katika maeneo ya mashambani dhidi ya wanyama wanaoweza kuhatarisha maisha yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.