ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 25, 2017

TETEMEKO LAUWA ASKARI MMOJA MKOANI MWANZA NA WAWILI KUPOTEZA FAHAMU

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi,


Tetemeko laua Mwanza
May 25, 2017

Tetemeko la ardhi lililotokea leo majira ya saa 6 na dakika 55 mchana mkoani Mwanza na kudumu kwa sekunde kama 30 hivi linadaiwa kusababisha kifo cha askari polisi kilichotokea wilayani Misungwi mkoani Mwanza. 

Akithiibisha kifo hicho Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema askari huyo amepatwa  na mkasa huo wakati akifanya mahojiano na mahabusu.
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA KAMANDA.

Marehemu askari Joyce  Mwalingo.
Aidha Kamanda Msangi amesema askari mwingine na mahabusu walipoteza fahamu na kupelekwa hospitali baada ya kupata taarifa za kufariki dunia kwa askari Joyce  Mwalingo.


Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi anawataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na hali yeyote ya dharura itakayojitokeza. BOFYA PLAY KUSIKILIZA MASHUHUDA WA MAENEO MENGINE JIJINI MWANZA.


Hili ni tetemeko la tatu kutokea mkoani Mwanza  katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja ambapo, Tetemeko la kwanza lilitokea septemba 5 mwaka jana likiwa na ukubwa wa 5.7. na tetemeko la pili lilitokea Aprili 30 mwaka huu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.