Na Abog
Baada ya kampuni ya michezo ya kubahatisha kutoka nchini
Kenya SportPesa kumwaga zaidi ya bilioni 10 kwa vilabu vya Simba na Yanga, leo
Mei 23 kampuni hiyo imetua rasmi katika klabu ya Singida United ambayo imepanda
daraja msimu huu.
Akiongea mbele ya waandishi wa habari kwenye Hotel ya
Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utawala na Uwezeshaji wa
kampuni hiyo Abbas Tarimba, amesema kuwa wana matumaini klabu hiyo italeata
changamoto kubwa kwenye ligi msimu ujao. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Mkataba huo una thamani ya shilingi milioni 250, kwa msimu
mmoja wa ligi ambapo wanatarajia kuongeza endapo timu hiyo itapata matokeo
mazuri kwenye ligi msimu wa 2017/18. Pia kuna makubaliano maalum ya nyongeza
(Bonus) endapo klabu hiyo itafuzu michuano ya kimataifa msimu ujao.
Kwa upande wa Singida United wamesema wana mipango ya
kufanya vizuri kwenye ligi ndio mana wameanza na usajili mzuri wa kocha pamoja
na wachezaji kutoka vilabu vikubwa barani Afrika kama Mamelodi Sondowns.
Moja
ya watu waliopo kwenye benchi la ufundi la Singida United ni nahodha Nizar
Khalfan ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga pamoja na kocha Hans Van Pluijm
ambaye naye amewahi kuinoa Yanga kwa mafanikio.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.