Wahitimu wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni Rasmi.
PICHA NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLINE
Shule ya Sekondari ya wavulana na wasichana ya WAJA imefanya
mahafali ya Kidato cha sita leo ambapo kwa upande wa Wasichana ni Mahafali ya Tatu na kwa wavulana ni ya Pili tangu
kuanza kwa Kidato cha Tano na cha Sita.
Jumla ya wahitimu 113 wamehitimu ambapo kwa upande wa shule ya wasichana ni
wanafunzi 79 na wavulana ni 34 ambapo ni katika michepuo ya sayansi na Sanaa.
Mafanikio ambayo yameweza kupatikana katika shule zote mbili
ni kutokana na kuwepo kwa taaluma ambayo inamwandaa mwanafunzi kuwa na uwezo wa
kujitegemea ambapo katika mitihani ya kanda ya ziwa shule ya wasichana ya WAJA
Girls ilishika nafasi ya 19 kikanda kati ya shule 57 na huku ikiwa ya tatu kati
ya shule 11 Mkoani Geita.
Kwa upande wa shule ya Wavulana ya WAJA ilishika nafasi ya
20 kikanda kati ya shule 57 huku wakishika nafasi ya 4 kati ya shule 11 zilizopo Mkoani Humo.
Hata hivyo kwa upande wa michezo shule Hizo zimeendelea
kufanya vizuri hali ambayo imesababisha kuboresha viwanja vya michezo .
Akihutubia Wanafunzi Kwenye Maafari hayo Mkuu wa Wilaya ya
Geita ambaye alikuwa ni Mgeni Rasmi Mwl,Herman Kapufi amewasisitiza wanafunzi
kuwa na mienendo ambayo ni mizuri pindi watakapo kuwa kwenye jamii zinazo
wazunguka na kuachana na tabia zinazoweza kuwasababishia kutokutimiza ndoto
ambazo wamejiwekea.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Taasisi za WAJA ambazo zinamiliki
shule hizo,Mhandisi Chacha Mwita ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa
kupunguza Tozo ambazo zinaonekana kuwa zinawakandamiza kama za vibao vya shule
ambazo zinaonesha sehemu ambayo shule inapatikana pamoja na swala la majengo
ambayo yamekuwa yakitozwa Fedha nyingi tofauti na matarajio ambayo wao
wanafanya shughuli zao ambapo kwa mwaka unakuta kodi wanalipa kiasi cha
sh,Milion 12 .
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
|
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.