Serikali ya Gambia imezuilia mali zinazomilikiwa na rais wa zamani wa nchi hiyo Yahya Jammeh, zikiwemo akaunti 86 za benki na majumba ya kifahari 131.
Waziri wa Sheria, Aboubacar Tambadou, aliwaambia waandishi wa
habarai jana Jumatatu katika mji mkuu Bajul kuwa, serikali imepata
idhini ya mahakama ya kuzuia mali hizo zilizoporwa na Jammeh, ambaye kwa
sasa yuko uhamishoni katika nchi ya Equatorial Guinea.
Amesema matokeo ya awali ya uchunguzi wao yanaonyesha kuwa, Jammeh alichota zaidi ya dola milioni 50 za Marekani, fedha za uma, katika Benki Kuu ya nchi kati ya mwaka 2006 na 2016.
Jammeh kabla ya kushindwa katika uchaguzi wa Disemba Mosi mwaka jana Gambia
Baada ya maji kumfika shingoni mapema mwaka huu, iliarifiwa kuwa rais huyo aliyeiongoza nchi hiyo ndogo ya magharibi mwa Afrika aliondoka nchini akiwa na dola milioni 11 pesa za umma pamoja na magari ya kifahari ya serikali ya nchi hiyo.

Baada ya kuingia madarakani, Rais mpya wa nchi hiyo Adama Barrow alimwamuru Makamu wake wa Kwanza, Fatoumata Jallow-Tambajang kuchunguza faili la wizi wa fedha za umma dhidi ya Yahya Jammeh, akisisitiza kuwa hatopewa kinga ya kutoshtakiwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.