KUNDI la kigaidi na kitakfiri la Daesh ISIS
limesema kuwa Rais Donald Trump wa Marekani ni mtawala mpumbavu ambaye
kwa mikono yake ataitumbukiza nchi hiyo katika maangamivu makubwa.
Msemaji wa kundi hilo la wakufurishaji, Abu Hassan al- Muhajer,
amenukuliwa na gazeti la Daily Mail akisema kuwa: "Hakuna ushahidi wa
ziada unaohitajika kuthibitisha kuwa Marekani inaongozwa na mwanasiasa
jahili, Trump ni mpumbavu asiyeelewa wala kufahamu chochote kuhusu
Syria, Iraq na hata Uislamu."Kadhalika msemaji huyo wa ISIS ametoa orodha ya majina ya Wamarekani elfu 8 pamoja na data zao, ambao wanapania kuwaua hivi karibu ndani na nje ya nchi.
Genge hilo la kigaidi limevunja kimya chake na kumshambulia moja kwa
moja Trump, siku chache baada ya mwanasiasa huyo mwenye misimamo ya
chuki na ubaguzi wa chama cha Republican kuitisha mkutano na maafisa wa
ngazi za juu wa usalama na intelijinsia wa Marekani, ili kupanga
mikakati ya kulitokomeza kundi hilo.
Ili kutilia nguvu matamshi ya Trump kuhusiana na kitendo cha Washington cha kuanzisha genge la kigaidi la ISIS wakati wa urais wa Barack Obama huko Marekani, mtandao wa WikiLeaks mapema mwaka huu ulisambaza mitandaoni mkanda wa sauti ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wakati huo John Kerry, wakati alipoonana na wajumbe wa makundi ya wapinzani wa serikali ya Syria tarehe 22 Septemba mwaka jana.
Kerry alikiri kuwa, lengo lao kuu la kuanzisha genge la kigaidi la Daesh (ISIS) ni kuipindua serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.