Wakimbizi wa Nigeria. |
WANAWAKE wakimbizi wa Nigeria wamefanya
maandamano wakati wawakilishi wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
walipokuwa wanatembelea kambi yao ya wakimbizi.
Shirika la habari la Ufaransa
limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, maandamano hayo yamefanyika
huko Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno la kaskazini mwa Nigeria
ambalo wakati fulani lilikuwa ni ngome kuu ya genge la Boko Haram.
Waandamanaji hao wamelalamika kwamba
mashirika na taasisi zinazosimamia misaada ya kibinadamu zinapora
misaada inayotolewa na kusababisha upungufu mkubwa wa chakula kwa
wakimbizi hao.
Wajumbe 15 wa Baraza la Usalama la Umoja
wa Mataifa wanatembelea nchi nne za Nigeria, Chad, Cameroon na Niger
kuangalia hali ya wakimbizi katika nchi hizo za Kiafrika.
Timu hiyo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ilianza safari yake kwa kutembelea kambi za wakimbizi za nchini Cameroon.
Ramani ya Nigeria. |
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, lengo la
ziara hiyo pamoja na mambo mengine, ni kukusanya taarifa za awali
kuhusiana na hali halisi ya mambo nchini Nigeria.
Wananchi wa Nigeria ambao wamelazimika
kukimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya genge la kigaidi la Boko
Haram, mara nyingi wamekuwa wakiilalamikia serikali ya Nigeria kwa
kufanya ufisadi na kupora misaada ya kibinadamu inayotumwa kwa ajili ya
wakimbizi.
Kundi la Boko Haram ambalo limetangaza
utiifu wake kwa genge la kigaidi la Daesh (ISIS) lilianzisha
mashambulizi yake mwaka 2009 nchini Nigeria na mwaka 2015 lilipanua
mashambulizi yake hadi katika nchi jirani za Niger, Cameroon na Chad.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.