MGOMO wa wafanyakazi katika viwanja vya ndege
na mashirika ya ndege barani Ulaya umepelekea kufutwa mamia ya safari
barani humo, hatua ambayo imesababisha usumbufu mkubwa kwa wasafiri.
Gazeti la Independet limeandika
kuwa, Shirika la Ndege la Britishi Airways leo limefuta safari zake 40
kutokana na mgomo wa wafanyakazi wa kitengo cha minara ya kuongozea
ndege cha Ufaransa pamoja na mgomo wa wahudumu wa ndege wa shirika hilo.
Inaelezwa kuwa, akthari ya safari hizo
za ndege zilizofutwa leo kutokana na mgomo huo ni za kati ya London na
miji ya Ufaransa. Mbali na Ufaransa, safari nyingine sita za ndege
zimefutwa leo zikiwa ni za kati ya Uwanja wa Ndege wa Heathrow wa mjini
London Uingereza na Barcelona Uhispania na vile vile Milan Italia.
Aidha safari za kutoka London kuelekea katika miji mikubwa mitatu ya Uswisi yaani Zurich, Basel na Geneva nazo zimefutwa leo kutokana na mgomo huo.
Aidha safari za kutoka London kuelekea katika miji mikubwa mitatu ya Uswisi yaani Zurich, Basel na Geneva nazo zimefutwa leo kutokana na mgomo huo.
Ndege ya Shirika la British Airways. |
Shirika la Ndege la Ufaransa Air France
nalo leo limelazimika kufuta safari zake nyingi za ndani za kutokea
Paris au za kuelekea katika mji mkuu huo.
Mgomo wa wafanyakazi wa kitengo cha
minara ya kuongozea ndege nchini Ufaransa unatarajiwa kuendelea hadi
tarehe 10 mwezi huu wa Machi. Wafanyakazi hao wamegoma wakilalamikia
kiwango kidogo mshahara.
Wafanyakazi hao wa kituo cha minara ya
kuongozea ndege nchini Ufaransa wanasema kuwa, wenzao walioko Ujerumani
wamekuwa wakilipwa mshahara mkubwa kuliko wao tena huku kazi zao zikiwa
ni chache ikilinganishwa na wao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.