RAIS Donald Trump wa Marekani amesaini
muswada wa kuondoa marufuku ya kununua silaha iliyokuwa imewekwa kwa
watu wenye ulemavu mkubwa wa akili.
Muswada huo uliosainiwa na Rais wa Marekani ulipitishwa siku
chache zilizopita na Baraza la Seneti kwa kura 57 dhidi ya 43
zilizoupinga.Kusainiwa muswada huo kumetajwa kuwa sehemu ya orodha ya mwisho ya miswada mipya iliyosainiwa na Trump. Utiaji saini huo umefanyika katika Ikulu ya White House pasina kuhudhuriwa na mwandishi yeyote wa habari.
Silaha moto zinauzwa kama bidhaa nyinginezo Marekani. |
Serikali ya Obama ilikuwa imetoa agizo kwa Idara ya Usalama wa Jamii kuyapatia maduka ya uuzaji silaha orodha ya majina ya watu wenye ulemavu mkubwa wa akili wanaotaka kununua silaha.
Kurahisisha ununuzi wa silaha moto ni moja ya ahadi alizotoa Trump wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais.
Jumuiya ya Kitaifa ya Silaha (NRA) imeunga mkono kupitishwa sheria hiyo na kueleza kwamba si watu wote taahira wanahesabika kuwa ni makatili.
Maelfu huuawa kila mwaka Marekani katika matukio ya ufyatuaji risasi. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.