ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 1, 2017

MVUVI AHOFIWA KUFA MAJI BAADA YA KUZAMA KATIKA ZIWA VICTORIA ENEO LA LUCHELELE.



MTU mmoja anahofiwa kufa maji baada ya kuzama katika ziwa Victoria katika eneo la Mtaa wa Soko kata ya Luchelele wilayani Nyamagana mkoa wa Mwanza.

Kabla ya kuzama katika ziwa hilo leo majira ya saa mbili asubuhi mtu huyo anayedaiwa kuwa alikuwa amelewa alikuwa ametoka kufanya biashara ya samaki kando ya ziwa hilo na kujaribu kuivuta mitumbwi yake miwili kuipeleka upande mwinginen ufukweni mwa ziwa hilo.

Mmiliki wa mitumbi hiyo Bi Grace Jackson anasema amepokea taarifa hizo akiwa katika shughuli zake nyingine.

Naye Mwenyekiti wa mtaa wa Soko kulipotokea tukio hilo Jummanne Madirisha amesema siyo mara ya kwanza kwa watu kupoteza maisha katika ukanda huo..

Afisa wa mtaa huo Fred Cherehani amewaasa wavuvi kutofanya shughuli za uvuvi hali ya kuwa wamelewa.

Juhudi za kulitafuta Jeshi la Polisi kuzungumzia tukio hilo bado zinaendelea.

BOFYA PLAY KUSIKIA KILICHOTOKEA (SAUTI KUWAJIA HIVI PUNDE)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.