ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 30, 2017

*TAARIFA YA ZUIO LA CAF KUHUSU MECHI YA YANGA KUCHEZWA UWANJA WA CCM KIRUMBA*

Ukaguzi.
 *TAARIFA YA ZUIO LA CAF KUHUSU MECHI YA YANGA KUCHEZWA UWANJA WA CCM KIRUMBA*

Uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba umeshangazwa na taarifa zilizoenea juu ya Zuio la CAF kwa Mechi ya Yanga na Mc Alger kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Kwanza, taarifa za awali za Mchezo hatukuzipata rasmi zaidi ya kuziona kwenye Mitandao kama wengine walivyoziona, hazikuwa rasmi kwa Uongozi wa Uwanja wala wamiliki wa Uwanja (CCM Mkoa wa Mwanza), na tarehe tajwa (8/04/2017) ilikuwa ni Tarehe itakayochezwa Mechi ya *Mbao FC Vs Simba FC* ambayo imesogezwa mbele Tarehe 10/04/2017 ( kwa taarifa tulizonazo) kutokana na tarehe ya awali kuingiliana na Shughuri nyingine za Kijamii ndani ya uwanja.

Pili, tangu taarifa imetoka juu ya Mechi hiyo Uongozi wa Uwanja ulikuwa umepokea Ugeni wa CAF kwa Ukaguzi wa Uwanja ambapo mpaka sasa Mkaguzi huyo bado yupo Mwanza amekuwa akifika mara kwa mara Uwanjani kukagua maendeleo ya Ukarabati ambao unapaswa Kukamilika Tarehe 10/04/2017 kwenye maeneo muhimu aliyoyaainisha.


Moja ya maeneo yaiyokuwa yakiharibu taswira ya uwanja ni eneo hili la mashariki (mbele ya jukwaa kuu) ni kichuguu ambacho sasa kimechimbuliwa na kutoa malkia wa kichuguu kisha udongo mpya ukawekwa hapa.
Hivyo, uongozi wa uwanja kama ulivyovieleza vyombo vya habari hakuna taarifa rasmi zilizokuwa zimefika juu ya Mechi hiyo ya Kimataifa kuchezwa katika uwanja wetu wa CCM Kirumba kama taarifa zilivyokuwa.


Mwisho, Uongozi wa uwanja wa CCM Kirumba kupitia Meneja wa Uwanja Ndg *Steven E. Shija* tunapenda kuwahakikishia Wadau wote wa Michezo ndani ya Mkoa wa Mwanza na nje ya Mkoa wa Mwanza kuwa, maelekezo yote yaliyotolewa na Mkaguzi wa CAF *Ndg Maxwell Mtoanga* yameanza kufanyiwa kazi siku ya pili sasa na yeye mwenyewe anafuatilia kwa ukaribu kila siku mpaka siku atakayoondoka Mkoani Mwanza Tarehe 30.03.2017.

*Imetolewa na:-*
*Uongozi wa Uwanja*
*CCM Kirumba - Mwanza*
*29.03.2017*

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.