Meneja Msaidizi wa Benki Kuu, (BoT) , kutoka
Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Bw.Abdul M. Dollah, akitoa mada juu ya
Huduma za Kibenki Benki Kuu ya Tanzania
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
IDADI
ndogo ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki kunachangia pakubwa kuchakaa
haraka kwa fedha.
Hayo
yamesemwa na Meneja Msaidizi wa Benki Kuu, (BoT) , kutoka Kurugenzi ya Huduma
za Kibenki, Bw.Abdul M.Dollah, wakati akijibu maswali ya Washiriki wa Warsha ya
Waandishi wa habari za Uchumi na Fedha, inayoendelea kwenye ukumbi wa BoT tawi la
Zanzibar, leo Machi 30, 2017 waliotaka kujua ni kwa nini fedha za noi
zinachakaa haraka hususan shilingi 500 na shilingi 1,000/_
“Ubora
wa karatasi zinazotumika kutengenezea noti zetu unalingana, lakini matumizi
makubwa ya noti hizo zilizotajwa, zinapita kwenye mikono ya idadi kubwa ya watu
na hivyo kupelekea kuchoka haraka.” Alifafanua
Akifafanua
zaidi alisema, Idadi ya Watanzania kwa sense iliyofanyika mwaka 2012 ni Milioni
48, lakini kati ya hao ni Watanzania Milioni 4 tu ndio wanatumia huduma za
kibenki, (kuwa na akaunti benki), na idadi ya waliosalia, hutunza wenyewe fedha
hizo.
Utunzaji
mbaya wa fedha na hali ya hewa ya baadhi ya maeneo nchini, huchangia kuchakaa
haraka kwa fedha “ Kwa mfano, kule Tanga maeneo ya Lushoto na Kibondo mkoani
Kigoma, kutokana na rangi ya udongo wa sehemu hizo, utakuta fedha inachakaa
haraka sana, alisema Bw.Dollah.
Akielezea
majukumu ya Kurugenzi ya Huduma
za Kibenki ya Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw. Dollah alisema, Sheria namba
Nne (4) ya BoT, imeipa kurugenzi hii jukumu la kusanifu, kutoa, kusambaza na
kuharibu fedha,(noti na sarafu), zilizochakaa.
Pia
Kurugenzi hii ina jukumu la kutoa huduma za kibenki kwa serikali zote mbili,
(Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi Zanzibar).
Alisema jukumu
lingine kubwa la Kurugenzi hiyo ni kuhakikisha uwepo wa noti na sarafu kwa
uwiano wa kutosha kwenye uchumi, “hatuwezi kuingiza fedha nyingi kwenye uchumi
bila ya kuangalia uwiano wa uzalishaji na kiwango cha fedha”.aliongeza.
Akizungumzia
kushuka na kupanda kwa thamani ya fedha ya Tanzania, (TZS), Mchumi Mwandamizi
wa BoT, kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, wa BoT, Bw. Lusajo
Mwankemwa, alisema, miongoni mwa sababu zinazopelekea hali hiyo ni uhitaji wa
fedha yetu, (TZS), katika soko(mzunguko).
“Ili
fedha yetu (TZS), iwe na thamani lazima uhitaji wake uwe mkubwa katika soko, na
ikitokea kwamba fedha yetu inahitajika kwa wingi basi fedha yetu itapanda
thamani na hii itatokana na kuongeza uzalishaji na kuuza bidhaa zetu nje,
lakini endapo uzalishaji utapungua, na Nchi ikaingiza kwa wingi bidhaa kutoka
nje, itapelekea uhitaji wa Shilingi kupungua na hivyo thamani yake pia
itapungua.” Alisema Lusajo. Na kushauri taifa kama taifa liongeze thamani ya
bidhaa ili ziweze kuuzwa nje na hivyo kuongeza uhitaji wa fedha yetu.
Aidha,
BoT, imesema, utafiti mdogo iliyofanya umeonyesha kuwa wateja wengi katika
benki za biashara, wanapokwenda kuchukua fedha, hupokea fedha (noti), za
thamani ya juu yaani 10,000, na 5,000 licha ya kuwa wengine wangependa kupewa
fedha ndogo ndogo kwa ajili ya urahisi wa kupata chenji.
“Ni haki ya mteja wa benki za biashara
anapokwenda kuchukua fedha benki, kudai apewe fedha za chenji (fedha ndogo
ndogo, yaani 500/- 1,000,000/ na 2,000/=, ili kumrahisishia anapokwenda kufanya
manunuzi asipate shida ya chenji.” Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na
Itifaki, Bi Vicky Msina alibainisha.
Washiriki wa semina, wakiangalia noti ya Sh. 10,000, ili kutambua kama ni halali au so halali.
Maafisa wa BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, (kulia), na Bw. Mohammed na Mohammed Kailwa, wakijadiliana jambo kwenye komppyuta
Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi.Vicky Msina, (kulia), akizungumzia kuhusu haki ya mteja wa benki ya biashara kupewa Fedha ndogondogo kama atahitaji. Kushoto ni Bw. Abdul M. Dollah.
Baadhi ya maafisa kutoka BoT
Mtangazaji wa Channel Ten, Bi. Dorcas R. Mtenga, akizungumza |
Bw. Dollah akitoa mada
Mchumi Mwandamizi
wa BoT, kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, wa BoT, Bw. Lusajo
Mwankemwa, akitoa ufafanuazi kuhusu kwa nini thamani ya shilingi ya Tanzania inapanda na kushuka
Bw. Dollah(kushoto), akiwa na Afisa Uhusiano Mkuu, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, BoT, Bw. Lwaga Mwambande
Maafisa wa BoT
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.