AFISA wa zamani wa Shirika la Usalama wa
Taifa la Marekani (NSA) amesema mifumo ya simu za iPhone na Android
inatumiwa na vyombo vya ujasusi vya Marekani kudukua na kunasa sauti na
mazungumzo ya watu katika maeneo mbalimbali ya dunia.
Jumanne ya jana mtandao wa WikiLeaks ulichapisha sehemu ya kwanza ya nyaraka na mafaili ya siri ya shirika la ujasusi la Marekani CIA katika majmui iliyopea jina la Year Zero. Nyaraka hizo za siri zinafichua kuwa, CIA imekuwa ikifanya ujasusi wa kunasa na kusikiliza mazungumzo ya watu wanaotumia simu za iPhone zinazotengenezwa na kampuni ya Apple na zile zinazotumia mifumo wa Android na Microsoft na vilevile televisheni za Samsung kwa ajili ya kufanya ujasusi na kudukua sauti na mazungumzo ya watu katika pembe mbalimbali duniani.
Afisa wa zamani wa Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani (NSA) Edward Snowden anasema kufichuliwa nyaraka hizo kunathibitisha tena kwamba, mashirika ya ujasusi ya nchi hiyo yanajasisi na kunasa sauti za watumiaji wa simu za kiganjani.
Afisa huyo wa zamani wa NSA alikimbia Marekani mwaka 2013 akiwa na rundo kubwa la nyaraka za siri za mashirika ya ujasisi ya nchi hiyo na kwa sasa amepewa hifadhi nchini Russia.
Edward Snowden. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.