ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 8, 2017

MASHABIKI WA SOKA WAUZUNGUMZIA UWANJA WA NYAMAGANA KABLA YA KUANZA KWA LIGI DARAJA LA 3 NGAZI YA MKOA HII LEO.

Kitenge Juma Kitenge mtaalamu wa masuala ya sheria za soka akizungumza na GSengo wa Jembe Fm Mwanza.
Uwanja wa Nyamagana tayari umekamilika eneo la kusakatia kabumbu li tayari kwaajili ya kulaki michezo mbalimbali, vipi wadau wanauzungumziaje uwanja huo.....BOFYA PLAY KUSIKIA WALICHOSEMA
Alex Mahagi ni mwamuzi wa soka toka Vodacom Premium League toka mkoa wa Mwanza akizungumza na GSengo wa Jembe Fm Mwanza.
Kombaini ya wachezaji toka timu mbalimbali Mkoani Mwanza wamejumuika hapa kuufanyia majaribio uwanja huu.
Maelekezo.
Maboresho kwa sehemu zenye mapungufu.
FIFA ikishirikiana na Halmashauri ya Jiji la Mwanza hatimaye wamefanikisha hatua hii ya safari ya ukombozi wa soka la mkoa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwaujumla kwani vipaji vingi vilikuwa vikizalishwa hapa kwenye dimba hili lililofungwa kwa takribani mwaka mmoja kupisha ukarabati., kabla ya kuingia kwenye utata na hatihati ya kubadilishwa matumizi.

Na kwa kipindi kirefu moja kati ya changamoto imekuwa ni upatikanaji wa uwanja mbadala utakaosaidizana na ule wa CCM Kirumba, hiyo ikiwa ni baada ya viwanja vingi muhimu mkoani hapa kuwa katika hali tete kimatumizi (viwanja kuwa vibovu) nao vijana wengi wakikosa mahala pa mazoezi na michuano mbalimbali ikishindwa kufanyika kutokana na viwanja vingine tegemeo kuwa na matumizi mengine kama mikutano ya siasa na shughuli nyingine za mikusanyiko ya kijamii.

Siku ya kwanza Waziri wa Utamaduni na Michezo alipozuru eneo hili kufanya ukaguzi wa ukarabati, pamoja na kutembelea uwanja huu, Nape aliwataka Wanamwanza kuutunza na kuuthamini kama sehemu ya moja ya maendeleo na ukuzaji vipaji.

Pia aliahidi kuhamasisha wadau mbalimbali na makampuni kusaidia zoezi la ujenzi wa majukwaa  ya mashabiki


Aidha, alisema Serikali itaendelea kuwekeza kwa kufanya ukarabati kwenye viwanja mbalimbali nchini ili kuviboresha na kusaidia kusukuma maendeleo ya michezo kwa haraka zaidi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.