NA K-VIS BLOG
RAIS
John Pombe Magufuli, amelipongeza Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO) kutokana
na kasi yake ya kusambaza umeme nchini hususan vijijini.
Rais
aliyasema hayo Machi 5, 2017 wakati akizindua Mradi wa ujenzi wa kituo cha
kupoza na kusambaza umeme wa 132kv mkoani Mtwara.
Mradi
huo utakamilika Mei 30, 2017 na kitahudumia mikoa ya Mtwara na Lindi na hivyo
kutatua kero ya upatikanaji umeme kwenye mikoa hiyo ambayo shughuli za kiuchumi
zimeongezeka sana. Awali kituo hicho kwa sasa kina uwezo wa 33kv.
“TANESCO
mmenifurahisha sana kwa kutekeleza vema ilani ya uchaguzi ya CCM, kwa
kuhakikisha wanachi kote nchini wakiwemo wa vijijini wanapatiwa umeme.”
Alisema.
Rais pia alisema, anatambua changamoto
zinazolikabili shirika hilo hususan madeni ya bili za umeme kwenye taasisi za
serikali.
"Ninaagiza,
wale wote wanaodaiwa bili za umeme na TANESCO, walipe madeni yao haraka,
vinginevyo muwakatie umeme." Alisema Rais.
Alisema
"Hata Ikulu kama inadaiwa we kata, najua pia kuna deni la shilingi Bilioni
162 Kule Zanzibar, nako kama hawatalipa kateni umeme. tunataka TANESCO
iharakishe kusambaza umeme kwa wananchi sasa wasipolipwa madeni watawezaje
kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi.?". Aliuliza Rais Magufuli. Aidha kutokana
na kufurahishwa na kasi ya TANESCO kusambaza umeme kwenye maeneo Mengi ya nchi,
amesema ofisi yake iko tayari kusaidia fedha pale itakapoonekana kuna mkwamo wa
kifedha katika utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya umeme.
Rais Magufuli(wapili kushoto), Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo(watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt.Alexander Kiaruzi, na Mwenyekiti wa CCC mkoa wa Mtwara, wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo hicho.
Rais akiandika kitu, wakati akiteta na Profesa, Muhongo wakati wa uzinduzi huo.
Rais akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO baada ya kupiganao picha.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akihutubia." Najua kule Zanzibar TANESCO inadai karibu shilingi Bilioni 162, nako kama hawatalipa kata umeme" Alisema Rais katika hotuba take.
Rais Magufuli na Mmiliki wa kiwanda cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote, (walioshika bendera), wakizindua safari za malori hayo ya kubeba saruji.
Rais Magufuli akipeana mikono na Alhaji Dangote
Rais akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi Wa malori ya Dangote.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.