ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 6, 2017

HATIMAYE KASISI ANAYEJIITA NABII HUKO KONGO DRC, AJISALIMISHA KWA POLISI BAADA YA KUMTUSI RAIS KABILA KUWA SIO RAIA WA NCHI HIYO.

Wafuasi wa Ne Muanda Nsemi wakiwa kaatika kanisa lake.
MBUNGE na kiongozi wa Kanisa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye pia anajitaja kuwa ni nabii wa Mungu, Bwana, Ne Muanda Nsemi, amejitokeza hadharani baada ya kuwa mafichoni kwa wiki kadhaa, kufuatia kanisa lake kuzingirwa na jeshi la polisi la nchi hiyo.
Polisi ya Kongo DR iliamua kumsaka mbunge huyo kutokana na matamshi yake ya uchochezi aliyoyatoa dhidi ya Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo.
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Katika matamshi ambayo amekuwa akiyakariri kumuhusu rais huyo, Nsemi anadai kuwa Kabila ni mgeni ambaye hatakiwi kuwa rais wa taifa hilo ka katikati mwa Afrika, kama ambavyo hata jina lake asili sio analolitumia hii leo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.