ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 7, 2017

WAKINA MAMA MWANZA WASEMA KUNA HAJA YA SERIKALI KUONA UMUHIMU WA KUWAONDOLEA VIKWAZO VINAVYOSABABISHA WASHINDWE KUENDESHA VIWANDA VIDOGO VYA USINDIKAJI WALIVYONAVYO.



NA ZEPHANIA MANDIA ,TAR.07/03/2017


MDAHALO WA WANAWAKE ULIOANDALIWA NA SHIRIKA LA LISILO LAKISERIKALI LA KIVULINI MKOANI MWANZA


Ili kufikia azma ya serikali ya kuwa Tanzania ya viwanda wanawake wajasiliamali mkoani Mwanza wameiomba serikali kuona umuhimu wa kuwaondelea vikwazo vinavyosababisha washindwe kuendeleza viwanda vidogo  vya usindikaji walivyonavyo.

Kumekuwepo na mlolongo mkubwa katika kufanikisha suala la usajili kutoka katika Mamlaka zinazohusika ikiwemo ile ya Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini TFDA jambo linalowakatisha tamaa ya kuendelea kufanya shughuli za uzalishaji mali.

Hayo yamebainishwa katika mdahalo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani na suala la msingi likiwa ni kujadili nafasi ya wanawake katika kufanikisha azma ya serikali ya kuifanya Tanzania ya viwanda.


Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini mkoani Mwanza Yassin Ally ametoa rai kwa serikali kufanya jitihada kuhakikisha wanawake wanafanikiwa katika kutekeleza kauli mbiu ya mwaka huu.

 

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mwanza Kiteto Kishuma amesema licha ya changamoto walizonazo wanawake lakini ametoa wito wa kuunda vikundi vya ujasiliamali katika kujiletea maendeleo.


Awali akizungumza katika mdahalo kuo mwakilishi kutoka Shirika la viwanda vidogo SIDO mkoani Mwanza Rose Kabanya amesema kwa kipindi kirefu wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu kwa wanawake katika Nyanja mbalimbali na yapo mafanikio ya kutosha.


Baadhi ya washiriki wa mdahalo huo wamesema ili kufikia azma ya serikali ya kuwa Tanzania ya viwanda wanawake wanatakiwa kupewa kipaumbele kwa kuondoa vikwazo vinavyokwamisha jitihada za kujiletea maendeleo.


Kila mwaka hufanyika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani inapofika Machi Nane  na  kauli mbiu ya mwaka huu hapa nchini ni Tanzania ya viwanda, wanawake ni msingi wa mabadiliko ya kiuchumi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.