SHIRIKA la kutetea haki za binadamu la
Amnesty International limetoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu
mashambulizi ya silaha za kemikali yaliyofanywa na serikali ya Sudan
dhidi ya raia katika eneo la Darful lililoko magharibi mwa nchi hiyo.
Katika ripoti yake mpya, Amnesty International imetaka
kufanyike uchunguzi kamili kuhusu mashambulizi ya silaha za kemikali
yaliyofanyika katika miezi ya Januari hadi Disemba mwaka uliopita wa
2016 katika jimbo la Darfur.Taarifa iliyotolewa na maafisa wa Umoja wa Mataifa imeashiria mashambulizi ya kinyama yaliyofanywa na jeshi la serikali ya Sudan katika eneo la Darfur na kusema kuwa, kushindwa kwa wajumbe wa Jumuiya ya Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW) kufanya uchunguzi kuhusu suala hilo kunatia aibu na fedheha kubwa.
Katika ripoti yake ya mwezi Septemba mwaka jana, Amnesty International ililituhumu jeshi la Sudan kuwa limetumia silaha za kemikali katika mashambulizi yake dhidi ya vijiji vya eneo la Jabal Murrah katika eneo la Darfur. Ripoti hiyo ilikadiria kuwa watu baina ya 200 na 250 waliuawa katika mashambulizi hayo ya silaha za kemikali na kwamba wengi wao walikuwa watoto wadogo.
Ripoti hiyo ilikuwa na picha za watoto wadogo walioathiriwa na mashambulizi ya silaha za kemikali ya jeshi la serikali ya Sudan na vilevile picha za satalaiti za vijiji vilivyoharibiwa na mashambulizi hayo.
Rais wa Sudan Omar al Bashir |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.