WANAWAKE wawili wanashikiliwa na Jeshi la polisi Mkoani hapa baada ya kukutwa wanasafirisha bhangi kilo 110 kwa ajili ya kuuza kinyume na Sheria.
Tukio hilo limetokea juzi February 5 mwaka huu saa 8 mchana kwenye kizuizi cha mamlaka ya mapato (TRA)Wilayani Magu ambapo Jeshi la lilitiliashaka gari namba T349 DBA aina Tata mali ya Msolasa lilokuwa likitokea Sirari kwenda Mwanza na kulisimamisha kisha kulifanyia upekuzi na kumkamata Angelina Patrick (50) Mkazi wa Sirari akiwa na bhangi kilo 40 zilizokuwa zimefungwa kwenye marobota manne.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Naibu Kamishina wa polisi Ahmed Msangi Mtuhumiwa mwingine ni Frola Lucas (65) Mkazi wa Sirari alikamatwa kwenye gari T.834 CZH aina ya Yutong mali ya kampuni ya Africa Raha lilokuwa likitokea na kukamata kilo 70 zikiwa zimefungwa kwenye marobota manne ndani ya masunduku matatu.
Aidha watuhumiwa wapo katika mahojiano na Jeshi la polisi na kwamba uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani huku askari wakiendelea na ukamataji wa magari wanayoyatilia shaka katika maeneo hayo.
Hata hivyo Kamanda Msangi amewataka wamiliki wa vyombo vya Moto kuacha tabia ya kujihusisha na usafirishaji Bhangi kwani ni kosa na endapo ikibainika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yao huku akiwataka wananchi wa Mkoa wa Mwanza kutoa ushirikiano ili kutokomeza biashara yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.