MAKALA
YAJUE MAADILI YA MADIWANI
Na James Timber, Mwanza
Kanuni za
Serikali za Mitaa, Mamlaka za Miji kuhusu Maadili ya Madiwani za mwaka 2000
ambapo Kanuni hizi zimeundwa chini ya Sheria za Serikali za Mitaa na Mamlaka za
Wilaya ya Mwaka 1982.
Nini maana ya Diwani?, Diwani ni Mjumbe wa Halmashauri
anayofanyia kazi.
Misimamo ya msingi, Kaulimbiu, Majukumu na
Malengo.
Kaulimbiu, Diwani atatakiwa
kuzingatia kaulimbiu ya Halmashauri inayoendesha shughuli zake kwa misingi ya
demokrasia na inayotekeleza majukumu yake kwa ufanisi, uaminifu, udhibiti na
kwa namna inayowajali wananchi wake.
Jukumu la
msingi, Diwani kwa kushirikiana na
madiwani wenzake, watumishi wa Halmashauri wa Umma kwa ujumla watafanya kazi
kwa lengo la kuhamasisha maendeleo endelevu ya kiuchumi katika Kata yake na
Katika eneo la Halmashauri.
Lengo, Lengo la Kanuni hizi za Maadili ni kufafanua Taratibu
za Mwenendo wa Madiwani utakaowawezesha
kutekeleza majukumu yao kwa namna itakayojenga na kudumisha imani ya umma kwa serikali zao za Mitaa.
Kanuni za maadili ya Madiwani, Wakati wote anakuwa na mwenendo mzuri kwa umma inayoweza kulinda imani kwa Halmashauri.
Anazingatia Sheria,
na kwamba wakati wote matendo yake yanaendana na dhamana aliyopewa na umma.
Diwani anaisaidia Halmashauri kwa kadri iwezekanavyo kuendesha shughuli zake kwa
kuzingatia maslahi ya jamii nzima ya Halmashauri ambayo anaifanyia kazi.
Diwani
hajiweki katika mazingira ambamo heshima na utu wake unatiliwa mashaka.
Aidha Diwani
anawajibika kwa wapiga kura wake na jamii yote ya Halmashauri kwa matendo yake na
kwa maamuzi yatakayofanywa na Halmashauri, kwamba Diwani anakuwa muwazi katika
matendo yake na kuyaelewa maamuzi ya Halmashauri na kuyasimamia.
Diwani
lazima afanye maamuzi bila ya upendeleo na bila kushawishiwa na mawazo ya watu wengine
hasa anapotekeleza shughuli za umma, na anaposhiriki uteuzi wa watumishi wa umma wakati wa kutoa mikataba
au wakati wa kutoa mapendekezo ya kutoa zawadi.
Diwani
atatunza siri, au taarifa atakazopata
zinazohusu watu binafsi zinazoshughulikiwa kwa kwa mujibu wa sheria au kwa
manufaa ya umma na hazitumiki kwa shughuli zake binafsi.
Marufuku
kutangaza maslahi yoyote ya binafsi yanayohusiana na utendaji wake wa shughuli
za umma wakati wa mkutano wa Halmashauri au wa Kamati ambayo yeye ni mjumbe.
Na mwisho
Diwani ataheshimu nafasi ya watumishi wa umma na Maofisa wa Halmahauri anayofanyia
kazi kama mjumbe, na kuwatendea namna ambayo inajenga heshima kwa pande zote.
Vigezo vya tabia binafsi, Kila Diwani atatakiwa;
Kuwa mtenda
haki, muwazi, mkweli, mwaminifu kitaaluma na kisiasa na asiwe na migongano ya
kimaslahi.
Kuendesha
maisha yake kwa namna itakayolinda heshima ya Halmashauri na kuinua imani ya umma kwa Halmashauri.
Kwa
madhumuni ya kuinua au kuongeza imani ya umma, Diwani anatakiwa kuzingatia
kiwango cha juu kabisa cha uadilifu
wakati anapokuwa Diwani.
Diwani
hatakuwa na uhusiano usioruhusiwa wa kimapenzi na Diwani mwenzake au mtumishi wa
Halmashauri.
Madeni na marafiki, Diwani hatakiwi kutumia vibaya dhamana
na imani aliyonayo kwa umma kama,
(a) kukopa
kwa kiwango kinachozidi uwezo wake wa kulipa madeni yake au kwa kiwango ambacho
kinamwondolea hadhi au kudhoofisha uwezo wake wa kutenda na kufanya maamuzi
yenye msimamo,
(b) kuwa na uhusiano na watu na tabia zenye
mashaka kwa namna inayoharibu mtazamo na imani waliyonao kwa Halmashauri.
charitytimberland@gmail.com
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.