ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 23, 2017

SIYO JAMBO LA KUFICHA TENA KUNA NJAA KUBWA AFRIKA NA YEMEN.


KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema baa la njaa limeenea katika nchi kadhaa za Afrika na Yemen huku akisema hali ya Sudan Kusini ni mbaya sana.

Akizungumza Jumatano katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari ukimjumuisha mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo UNDP Helen Clark, mratibu wa masuala ya binadamu wa Umoja wa Mataifa Stephen O'Brien na wadau wengine wakiwemo WFP, FAO na UNICEF amesema kikao hicho kimeitishwa kuufahamisha ulimwengu hali halisi ya njaa.

Guterres ameonya kwamba hali ni mbaya na dunia isipoziba ufa basi italazimika kujenga ukuta na kuongeza kuwa: "Leo hii watu zaidi ya milioni 20 Sudan Kusini , Somalia, Yemen , na Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wanakabiliwa na njaa na hawana uhakika wa chakula".

Amesema endapo hatua hazitochukuliwa hivi sasa basi muda si mrefu hali hii itayakumba pia maeneo na nchi zingine.



Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa kimataifa na mashirika ikiwemo Bank ya dunia watafanya kila liwezekanalo kunusuru maisha ya watu kukiwemo kuundwa kwa kamati itakayokuwa daraja baina ya Umoja wa Mataifa na mashirika mengine lakini kwamba wanakabiliwa na changamoto kubwa.


Guterres ameonya kuwa moja ya vikwazo vikubwa ni fedha za ufadhili na kuongeza kuwa operesheni za kibinadamu katika nchi husika kwa muda wa miaka manne zinahitaji zaidi ya dola bilioni 5.6. Amesema kwa mwaka mashirika ya kutoa misaada yanahitaji angalau dola bilioni 4.4 ifikapo mwisho wa Machi ili kuepuka maafa

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.