TAREHE
01.02.2017 MAJIRA YA SAA 16:00HRS JIONI KATIKA ENEO LA MSITU WA HIFADHI YA SERIKALI
WA BUHINDI ULIPO KIJIJI CHA ILYAMCHELE TARAFA YA BUCHOSA WILAYA YA SENGEREMA
MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA PAMOJA NA MAAFISA WA HIFADHI YA MSITU WA SERIKALI
YA BUHINDI WALIFANIKIWA KUTEKETEZA SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA EKARI MBILI NA
NUSU AMBALO LILIKUWA NDANI YA HIFADHI HIYO.
POLISI WALIPOKEA
TAARIFA ZA UWEPO WA SHAMBA HILO LA BHANGI KUTOKA KWA MAAFISA WA HIFADHI YA MSITU
HUO, NA KWAMBA WANANCHI AMBAO WANAOISHI KARIBU NA MSITU NDIO WALIOPANDA BHANGI
HIYO KATIKA ENEO HILO NA PINDI WANAPOKATAZWA WAACHE TABIA HIYO WAMEKUWA
WAKIKAIDI NA KUWATISHIA KUWAPIGA KWA MAWE MAAFISA WA HIFADHI HIYO. ASKARI
WALIKWENDA PAMOJA NA MAAFISA HAO HADI ENEO LA HIFADHI YA MSITU NA KUKUTA ENEO
LA EKARI MBILI NA NUSU LIKIWA LIMEOTESHWA BHANGI, ASKARI KWA KUSHIRIKIANA NA
MAAFISA WA HIFADHI YA MSITU WALIFANIKIWA KUTEKETEZA SHAMBA HILO LA BHANGI
LILILOKUWA NA JUMLA YA IDADI YA MICHE 7300 YA BHANGI. POLISI BADO WANAENDELEA
NA UPELELEZI ILI KUWEZA KUWABAINI WATU AMBAO WALIHUSIKA NA KUOTESHA BHANGI
KATIKA ENEO LA MSITU WA HIFADHI YA SERIKALI WA BUHINDI.
AIDHA KATIKA TUKIO
LINGINE LA TAREHE 02.02.2017 MAJIRA YA SAA 06:00HRS ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA
KAFUNZO KILICHOPO WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, ASKARI
WAKIWA KWENYE MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA
MKORO MSAMI MIAKA 74, MKAZI WA KIJIJI CHA MAFUNZO, KWA KOSA LA KUOTESHA MICHE
84 YA BHANGI KWENYE SHAMBA LENYE UKUBWA WA EKARI MOJA NA NUSU, KITENDO AMBACHO
NI KOSA KISHERIA.
AWALI POLISI WALIPOKEA
TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA JUU YA UWEPO WA MTU KATIKA KIJIJI TAJWA HAPO JUU
ANAYEJIHUSISHA NA KILIMO CHA BHANGI, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI JUU YA
TAARIFA HIZO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA PAMOJA NA SHAMBA LAKE NA KUANZA
ZOEZI LA KUNG’OA MICHE YOTE YA BHANGI
KATIKA SHAMBA HILO KISHA KUITEKETEZA KWA MOTO.
MTUHUMIWA YUPO KATIKA
MAHOJIANO NA ASKARI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIAKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, POLISI
WANAENDELEA NA UPELELEZI PAMOJA NA
MISAKO KATIKA MAENEO YOTE ILI KUWEZA KUWAKAMATA NA KUWADHIBITI WATU WOTE
WANAOJIHUSISHA NA KILIMO HARAMU CHA BHANGI.
KAIMU KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO SENGA ANATOA WITO KWA
WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA
JESHI LA POLISI, ILI LIWEZE KUWAKAMATA NA KUDHIBITI WATU WOTE AMBAO
WANAJIHUSISHA NA KILIMO HARAMU CHA BHANGI NA KUWAFIKISHA KATIKA VYOMBO VYA
SHERIA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.