ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 14, 2017

WASIRA HAKUBALI KUSHINDWA, ARUDI TENA MAHAKAMANI.

NA ANNASTAZIA MAGINGA,
GSENGO BLOG Mwanza
ALIYEKUWA mgombea ubunge Jimbo la Bunda Mjini (CCM) kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015 Stephen Wasira, hakubali kushindwa  mara baada ya wapiga kura wanne ambao ni Magambo Masato,  Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila, kukata rufaa katika Mahakama ya rufaa kwa ajili ya kupinga matokeo ya ubunge  wa Jimbo  hilo  dhidi ya  Ester Bulaya (Chadema).

Aidha Mwaka jana  Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, ilimtangaza Ester Bulaya (Chadema) kuwa mbunge halali wa Jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara baada ya kumshinda Wassira kwa mara ya pili dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa Novemba 19 mwaka 2015 kwa mara ya kwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi ofisini kwake, naibu msajili Mfawidhi katika mahakama kuu ya Mwanza Francis Kabwe, ameeleza  kesi hiyo inaanza kusikilizwa   Februari 20, mwaka huu.

Kabwe amesema  kuwa kwa mjibu wa katiba ya Tanzania mtu ambaye anashindwa mara ya mwisho kwenye mahakama ya Rufaa ndo mwisho anapaswa kukubali kushindwa na kuheshimu maamuzi ya mahakama.

“Hapa ndo mwisho atakayeshindwa lazima akubaliane na matokeo  maana ndo inakuwa mwisho wa rufaa, hivyo mheshimiwa hapa ikila kwake basi ndo basi tena hamna namna inabidi basi ajipange kwenye miaka mingine”, alisema Kabwe.

Amesema  kesi itakuwa chini ya jopo la majaji watatu ambao ni Justice Ibrahimu, Justice Mabrouk, na jaji Mwalija, ambapo pia alisema wanaweza kubadilishwa kutokana na majukumu mengine ya kikazi.


aidha awali  kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa novemba mwaka 2015 mahakama kupitia  Jaji Chocha alimtangaza Bulaya kuwa mbunge halali wa Jimbo la Bunda Mjini, na kueleza kuwamlalamikaji namba 1, Magambo Masato na mlalamikaji namba 2 wa kesi hiyo, Matwiga Matwiga, wao walikuwa watalii tu mahakamani hapo na si walalamikaji.


Jaji huyo aliianisha msingi wa kesi hiyo ambayo awali ilitupiliwa mbali Mahakama hiyo, kabla ya Mahakama ya Rufaa kuirejesha tena mahakamani kusikilizwa upya, Jaji Chocha alisema walalamikaji walikuwa wakiomba kubatilishwa kwa matokeo yaliyompa ushindi Bulaya, huku wakiomba  kuhesabiwa kwa kura upya , Mahakama kuamuru kurudiwa upya kwa uchaguzi wa ubunge Jimbo hilo la Bunda Mjini. 

Hata hivyo Katika uchaguzi huo, Msimamizi wa Uchaguzi aliiambia Mahakama kuwa Stephen Masato Wasira, alipata kura halali 19,126 na Ester Amos Bulaya, yeye alipata kura halali 28,568 alizopigiwa na wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.