ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 3, 2017

MWANADIPLOMASIA WA SAUDIA APATIKANA NA HATIA YA KUBAKA, KULAWITI.


MAHAKAMA moja nchini Singapore imempata mwanadiplomasia wa Saudi Arabia, na hatia ya kubaka na kulawiti mhudumu mmoja wa hoteli kusini mwa nchi hiyo ya bara Asia.
Bander Yahya al-Zahrani, mwanadiplomasia wa Saudia mjini Beijing anakabiliwa na mashitaka matatu ya ubakaji, liwati na kumdhalilisha kijinsia mhudumu mmoja wa hoteli mwenye umri miaka 20, Agosti mwaka jana 2016.
Lee Poh Choo, Jaji wa Mahakama ya Wilaya aliyeisikiliza kesi hiyo jana Jumatano amekataa ombi la wakili wa mwanadiplomasia huyo, la kutaka kesi hiyo itupiliwe mbali kwa kuwa mteja wake anadai kuwa mhudumu huyo wa hoteli alishirikiana na wasimamizi wa hoteli hiyo ili kumhadaa ili kumpora pesa.
Mwanadiplomasia huyo wa Saudi Arabia anadaiwa kumnajisi na kumlawiti mhudumu huyo mnamo Agosti 14 mwaka jana, alipokuwa ameenda likizo katika kisiwa cha Sentosa, nchini Singapore.
Wanawake wakiandamana India kupinga kinga ya kisheria kwa mwanamfalme mbakaji wa Saudia

Hukumu dhidi ya mwanadiplomasia huyo wa utawala wa Aal-Saud inatazamiwa kutolewa kesho Ijumaa, na huenda akahukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela au faini ya dola 1,500 za Marekani kwa kumdhalilisha kijinsia binti huyo wa miaka 20, na pia kifungo cha miaka 10 kwa shitaka la kulawiti.
Oktoba mwaka jana, mwanadiplomasia mwengine wa Saudia alituhumiwa kuwabaka wanawake wawili wa Nepal waliokuwa wakifanya kazi katika makazi yake mjini New Delhi nchini India.
Aidha Oktoba mwaka 2015, wanawake watatu katika jimbo la Los Angeles nchini Marekani waliodhalilishwa kijinsia na mwanamfalme wa Saudia, Majid bin Abdulaziz Al Saud waliwasilisha mashtaka yao mahakamani nchini humo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.