ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 13, 2017

MAKONDA AKABIDHI MAJINA 97 YA WATUHUMIWA DAWA ZA KULEVYA KWA KAMANDA SIRO.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akionesha faili la majina mengine 97 ya wauza Dawa za kulevya awamu ya tatu kwa kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kuzuia na Kupambana na Dawa za kulevya Bw. Rogers William Sianga ili yaanze kushughulikiwa .
Dar es salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo ameamua kutokutaja majina 97 ya watuhumiwa dawa za kulevya badala yake ameyakabidhi kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro ili ashughulike nayo.

Akizungumza leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Makonda ambaye awali alitaka majina zaidi ya 70 katika makundi mawili, amesema ana imani Siro atayashughulikia ipasavyo wahusika.


Mbali na hilo Makonda ameyamulika maduka ya kubadilishia fedha na viwanja vya ndege kuwa vinatumika kutakatisha fedha za dawa za kulevya.        

             
“Viwanja vya ndege mamilioni yanapita na hakuna msisitizo wa kukomesha, tushirikiane katika hili kukomesha , mkoa mmoja zipo Bureau De change zaidi ya 220. Wakati tunatumia fedha za ndani badala ya dola, nchi nzima zipo 400,” amesema.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.