ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 13, 2017

BUNDUKI ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI YANASWA NYUMBANI KWA MTU MWANZA.


JESHI la polisi mkoani Mwanza linamshikilia mama mmoja mmiliki wa nyumba Bi. Bigire Kalemani kwa mahojiano Zaidi mara baada ya kukutwa nyumbani kwake silaha moja moja iliyotengenezwa kienyeji aina ya gobole.
Tarehe 12.01.2017 majira ya saa 4 asubuhi katika mtaa wa Kabangaja kata ya Sangabuye mkoani Mwanza Silaha moja iliyotengenezwa kienyeji aina ya gobole inayotumia baruti imekamatwa kwenye chumba nyumbani kwa Bigire Kalemani  (42) mkazi wa mtaa wa Kabangaja ikiwa imefungwa kwenye mfuko wa sandarusi na kufukiwa ardhini kisha juu kupangwa matofali, kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Inatajwa kuwa majira tajwa hapo juu Mwanamke mmoja aitwaye Asha Bisco (35) alikuwa akifanya usafi chumba chake alichopangisha kilichopo kwenye nyumba ya mwanamke tajwa hapo juu ili aweze kuhamia, aidha inadaiwa wakati akiendelea na usafi aliona mfuko wa sandarusi chini ya ardhi akijua ni uchafu ili akatupe, ndipo baada ya kuutoa mfuko huo na kuuangalia ndani aliona silaha hiyo aina ya gobole.

Mara baada y akuikuta silaha hiyo mahali hapo Bi. Asha Bisco aliamua kutoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo, askari walikwenda haraka hadi eneo la tukio na kufanikiwa kuikata silaha hiyo.
Tayari mama mwenye nyumba Bi. Bigire Kalemani anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano Zaidi juu ya kupatikana kwa silaha hiyo hapo nyumbani kwake, nao upelelezi ukiendelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kuepusha madhara.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.