Akitoa ufafanuzi juu ya utaratibu wa uchukuaji ruzuku kwa kaya isiyo kuwa na mama Maxmilian amesema mtu yeyote msimamizi wa kaya anaruhusiwa kuchukuwa ruzuku endapo serikali ya kijiji ikishakudhibitisha na endapo amefariki kuna utaratibu wa kubadilisha msimamizi
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA Mratibu wa Tasaf
Akizungumza na wananchi hao afisa maendeleo alimashauri ya wilaya ya sengerema Bwana Bushaija amewataka kuzitumia fedha hizo kwa maendeleo kwa kuanzisha miradi midogo na kwawanao pata ruzuku kupitia watoto wanaosoma kuhakikisha wamapelekwa shule.
Kwaupande wake afisa elimu sekondari bwana Godwin Barongo amesema kuwa watoto walioandikishwa kwenda shule wote waende shulena endapo mtoto hatakwenda shule pesa ya ruzuku itapugua na kuongeza kuwa pesa hizo zisaidie kuwanunulia mavazi ikiwemo sale za shule
Akizungumzia changamoto wanazokutana nazo mjumbe wa serikali ya kijiji Bi Debora Clifod amesema changamoto ni kwa walengwa wasiofika siku ya utoaji ruzuku kutokana na dharula mbalimbali pesa zao kurudisha na mwezi unaofuata hawapatiwi
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA Debora Clifod
Akijibu kuhusu changamoto mratibu wa tasaf alimashauri ya Sengerema amesema kuwa fedha zote ambazo hazijalipwa katika muda husika yanarudi katika kipindi cha malipo yanayofuata ingawa amekili kuwa siku awali kulikuwa na changamoto katika utendaji kwasasa changamoto hiyo imeshakwisha.
Bi Salome Andrea na bwana Emanueli Masanja ni wadau wa ruzuku kwa upande wake bi Salome amesema kuwa tangu amepata ruzuku amefanikiwa kununua mifugo,mavazi ya watoto na chakula.Akiishukuru tasafu Emanuel Masanja amesema kuwa amefanikiwa kujenga nyumba imara na kuwapeleka watoto shule na kuanza ufugaji
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.