TAARIFA
YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA
HABARI LEO TAREHE 11.01.2017
·
MTU
MMOJA AMEUAWA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA KUTENDA
WIZI WA NJIA YA MTANDAO WILAYANI ILEMELA.
TAREHE
10.01.2016 MAJIRA YA SAA 17:00HRS KATIKA KIJIJI CHA IGOMBE KATA YA BUGOGWA
WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA MWANAMUME ALIYEJULIKANA KWA
JINA LA EDSON PAUL MIAKA 24, MSUKUMA NA MKAZI WA BUSWELU, ALIUAWA NA KUNDI LA
WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA KUTENDA WIZI KWENYE DUKA LA MIHAMALA YA FEDHA YA NJIA YA MTANDAO.
INADAIWA KUWA MAREHEMU
ALIFIKA KWENYE DUKA LA MIHAMALA YA FEDHA (M-PESA, TIGO PESA, AIRTEL MONEY) NA
KUMWOMBA MHUDUMU WA DUKA HILO AITWAYE BAHATI NYAGAWA MIAKA 18, AMTUMIE FEDHA
KWA NJIA YA M-PESA KIASI CHA TSH 295,000/=, KWENYE NAMBA YAKE YA SIMU,
INASEMEKANA KUWA BAADA YA KUTUMIWA FEDHA HIZO KWENYE NAMBA YAKE YA SIMU MHUDUMU
WA DUKA HILO BAHATI NYAGAWA ALIOMBA KUPATIWA FEDHA HIZO (CASH) AMBAZO
ALIMHUDUMIA, MAREHEMU ALIONEKANA HAKUWA NA FEDHA NA ALITAKA KUTOROKA ENEO LA
TUKIO.
INASEMEKANA KUWA WAKATI
ANATAKA KUTOROKA ENEO LA TUKIO, WANANCHI WALIOKUWA MAENEO YA KARUBU WALIJITOKEZA
NA KUMKAMTA NA KUANZA KUMSHAMBULIA KWA
MAWE NA MARUNGU SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE HADI UMAUTI UKAMKUTA PAPO HAPO.
JESHI LA POLISI
LINAMSHIKILIA MHUDUMU WA DUKA HILO BAHATI NYAGAWA KWA MAHOJIANO ZAIDI, AIDHA
HAKUNA MTU MWINGINE YEYOTE ALIYEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO, MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI,
PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA RAI KWA WAKAZI WA JIJI
NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI
NI UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU, BALI
WAFUATE UTARATIBU PINDI WANAPOMKAMATA MHALIFU ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA
ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE.
AIDHA ANAWATAKA VIJANA KUFANYA KAZI ZA HALALI NA
KUACHA TABIA ZA UHALIFU KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI. ENDAPO MAREHEMU
ASINGEFANYA TUKIO HILO HAYA YALIYOMKUTA YASINGEMPATA.
MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NOTI BANDIA WILAYANI ILEMELA.
MNAMO TAREHE 11.01.2017
MAJIRA YA SAA 01:30HRS, USIKU KATIKA MAENEO YA KISS PUB KATA YA KIRUMBA WILAYA
YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA DORIA NA MISAKO WALIMKAMATA
MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA JAMES PETER MIAKA 22, MKAZI WA MISUNGWI AKIWA
NA NOTI BANDIA NNE ZA SHILINGI ELFU KUMI YA TANZANIA ZENYE TAHAMANI YA JUMLA YA
TSH, 40,000/=, ZENYE NAMBA 1. BX 98546121, 2. BX 9851404, 3. BX 9851407 NA 4.
BX 320598, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
AWALI ASKARI WALIPOKEA
TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA JUU YA UWEPO WA KIJANA MWENYE FEDHA BANDIA MAHALI
HAPO, ASKARI WALIKWENDA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUFANYA UPELELEZI
KUHUSIANA NA TAARIFA HIZO NA KUFANIKIWA KUMTIA NGUVUNI MTUHUMIWA TAJWA HAPO
JUU. TUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANA NA JESHI LA POLISI, PINDI UCHUNGUZI
UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA
JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA
POLISI ILI LIWEZE KUWAKAMATA WAHALIFU KATIKA MKOA WETU WA MWANZA, LAKINI PIA
ANAWATAKA WANANCHI KUBADILIKA NA KUFANYA KAZI ZILIZO HALALI.
IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M)
MWANZA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.