Ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) imeonesha kuwa, sera za kupambana na sigara na tumbaku ikiwa ni pamoja na kuweka ushuru na kodi kwa bidhaa hizo na kuzidisha bei zake vinaweza kudhamini pato kubwa kwa ajili ya sekta ya afya na maendeleo.
Oleg Chestnov ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa WHO amesema kuwa, hatua kama hizo zinaweza kupunguza sana kiwango cha utumiaji wa tumbaku na hivyo kuwalinda afya ya mamilioni ya watu duniani mbele ya wauaji wakubwa zaidi duniani yaani saratani na maradhi ya moyo.
Ripoti ya WHO imeongeza kuwa, kupandishwa bei ya bidhaa zinazotokana na tumbaku kunaweza kunyanyua juu kiwango cha afya ya walimwengu na kuokoa mabilioni ya dola za uchumi wa duniani.
Ripoti hiyo imeashiria uchunguzi uliofanyika mwaka jana na kusema kuwa: Iwapo nchi zote zitazidisha senti 80 tu kwa kila sigara moja mapato ya ushuru wa sigara duniani yanaweza kuongezeka kwa asilimia 47 yaani dola bilioni 140.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Shirika la Afya Duniani, karibu watu milioni sita hufariki dunia kila mwaka kutokana na utumiaji wa tumbaku na sigara.
Wakati WHO ikitangaza vita madhubuti dhidi ya sigara nchini Tanzania Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikwisha tangaza vita dhidi ya kaka wa sigara mwenye madhara makubwa zaidi hapa nazungumzia uvutaji wa Sheesha katika maeneo yote ya Jiji la Dar hali iliyo sababisha vita hivyo kuenea maeneo yote nchini na tamkohilo kuchukuliwa kama tamko la kitaifa.
MAKONDA NAYE ANAINGIA KWENYE HISTORIA.
Matumizi yake yalianzia mashariki ya kati lakini sasa imeenea mabara yote Duniani.
Nchini Tanzania watumiaji wakubwa ni vijana wa kike na kiume na watu wazima, Madhara kiafya kwa sababu ya sumu za aina tofauti zilizomo ndani ya moshi wa tumbaku na madawa mengine. Sheesha inaweza pelekea kupata Ugonjwa wa Saratani, magonjwa ya moyo, magonjwa ya ngozi, fizi za meno, kupugua kinga ya mwili, wajawazito kujifungua njiti na watoto wenye uzito mdogo, kuwa tegemezi na ngozi kusinyaa.
Mbaya zaidi Sasa hivi watu wanachanganya na madawa ya kulevya, ambayo ni madhara makubwa kiafya. Falme za kiarabu na nchi nyingine kama Uganda wamepiga marufuku matumizi ya Sheesha, kwani Hakuna faida yoyote ya kuvuta sheesha na inaangamiza vijana na kupunguza nguvu kazi ya taifa na kwenda kinyume na malengo ya Serikali ya awamu ya 5 ya Bwana JPM aliye madarakani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.