ASASI isiyo ya kiserikali ya Tusaidiane Mwaloni Kirumba wilayani Ilemela mkoani hapa (TMK) imeendesha kongamoano la siku tatu kwa wananchi na wakazi wa wilaya hiyo ili kuwajengea uwezo wa ushiriki katika bajeti ya maendeleo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo Mwenyekiti wa asasi hiyo Faustine Lugangila amesema kongamano hilo linalengo la kuwajengea uwezo wananchi juu ya kuhoji bajeti kwenye serikali za mitaa.
Lugangila amesema kongamao hilo limehusisha wenyeviti wa mitaa, maofisa watendaji, madiwani kutoka baadhi ya kata za Kitangiri, Kayenze Ilemela Pamoja na Buswelu zote za wilayani humo.
"ikiwa jamii itashilikishwa kwa ufasaha katika upangaji wa bajeti maendeleo yanapatikana kwa wakati unaohitajika ukilinganisha na sasa ambao wanaokaa kwenye vikao ni watendaji na madiwani pekee yao"amesema Lugangila
Aidha mwenyekiti huyo amewataka madiwani wote kuwashilikisha wananchi katika vikao vyao vya halmashauri ili kupatia taarifa muhimu za maendeleo kwenye maeneo yao.
Kwa upande wake mratibu mkuu wa semina hiyo Athanas Evarist ameeleza kuwa baadhi ya wananchi wameshindwa kushiriki kwenye mabaraza ya halmashauri licha ya kuwa wazi.
Pia amewaasa wananchi kujenga tabia ya kuudhulia vikao hivyo ambavyo ni muhimu kwa kuwasaidia kujua mipango ya maendeleo katika maeneo yao ikiwa na kutoa maoni yao.
" wananchi wanatakiwa kufuatilia mbao za matangazo ili kuweza kujua taarifa mbalimbal za mitaa ikiwa pamoja na kupata ratiba kamili ya kushiriki kwenye vikao hivyo.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa sabasaba Kichomnge Mwita aliziomba taasisi nyingine ziige mfanop wa TMK ili kuweza kutoa semina na elimu kwa wananchi ili kuweza kufuatili shughuli za maendeleo kwa watendaji wao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.