ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 9, 2017

UKATILI WA KUTISHA WA POLISI WA MAREKANI DHIDI YA MWANAFUNZI WA KENYA.

Kitendo cha ukatili kukiwemo kupigwa vikali na kutusiwa matusi machafu na polisi wa Marekani dhidi ya mwanafunzi mmoja mwenye uraia wa Kenya, kimemlazimu hakimu wa mahakama ya federali kutaka kuchunguzwa kitendo hicho.
Mashitaka ya Justin Muchama ni yenye kurudi nyuma hadi miaka mitatu iliyopita. Katika kipindi hicho maafisa wawili wa polisi wa kitengo cha uhamiaji walitumia nguvu na ukatili wa kutisha dhidi ya Muchama aliyepelekwa jela ya mji wa Butler, jimbo la Kansas kwa tuhuma za kukataa kuchukuliwa alama ya vidole miaka mitatu iliyopita. Kwa mujibu wa maafisa usalama wa jimbo la Kansas, Muchama anatakiwa kuondoka Marekani mara moja kutokana na kumalizika viza yake ya kuishi nchini humo.
Sehemu ya ukandamizaji wa polisi wazungu dhidi ya watu weusi nchini Marekani

Baada ya miaka mitatu kupita Cathirine Waratil ametupilia mbali pendekezo la serikali la kutaka kutochunguzwa maafisa wa usalama waliohusika na ukatili huo, na badala yake ametaka faili la ukatili huo lichunguzwe kwa kina na mahakama. Kwa mujibu wa Waratil, Muchama hakuwa tishio kwa usalama wa taifa na hivyo, kitendo cha askari hao kutumia nguvu kupindukia dhidi yake, hakikubaliki. Mwanafunzi huyo mwenye asili ya Kenya amesema kuwa, kipigo alichopigwa na askari hao kimemfanya kila wakati awe anaumwa kichwa na kupatwa na msongo wa mawazo. Itafahamika kuwa, hadi sasa Muchama bado anashikiliwa katika jela ya Butler nchini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.