WATU zaidi ya milioni moja nchini Uingereza wamesaini ombi la malalamiko wakiitaka serikali ya nchi hiyo kufuta mwaliko wa Rais Donald Trump wa Marekani kwenda London kwa ajili ya kuonana na Malkia Elizabeth wa nchi hiyo.
Ombi hilo la kutaka kuzuia safari ya Trump huko London lilianza kuafuatiliwa mwezi Novemba mwaka jana, miezi kadhaa kabla ya Theresa May, Waziri Mkuu wa Uingereza kuizuru ikulu ya Marekani White House hivi majuzi.
Akiwa ziarani nchini Marekani, Theresa May aliwasilisha mwaliko huko kwa Trump kwa ajili ya kufanya ziara rasmi nchini Uingereza. Kampeni ya kuzuia safari ya Rais wa Marekani mjini London ilishika kasi baada ya Donald Trump kutoka chama cha Republican kusaini marufuku ya siku tisini inayowazuia kuingia nchini humo raia wa nchi saba za zenye Waislamu wengi.
Donald Trump anatazamiwa kuitembelea Uingereza baadaye mwaka huu.
Hadi kufikia sasa ombi hilo limeshasainiwa na watu zaidi ya milioni moja. Wabunge wa Uingereza wanapasa kulizingatia ombi ili kulijadili iwapo kutapatikana saini zaidi ya milioni moja la kuliunga mkono.
Wakati huo huo Wabunge wa chama tawala cha Conservative na wale wa upinzani wa chama cha Labour wamekosoa hatua hiyo ya Rais wa Marekani huku mkuu wa chama cha Labour, Jeremy Corbyn akisema kuwa, safari ya Trump nchini humo inapasa kufutwa.
Maandamano ya kupinga hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuwazuia Waislamu kutoka nchi saba yaani Iraq, Iran, Sudan, Yemen, Syria,Jordan na Somalia kuingia Marekani yanaendelea kushuhudiwa nchini Marekani kwenyewe na katika nchi nyingine duniani.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.