JESHI la Polisi mkoani hapa, linamshikilia mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Eveline John (24) mkazi wa Butuja kwa kosa la Kumtupa mtoto wake mchanga katika ziwa Viktoria mara baada ya kujifungua.
Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 8 majira ya saa 10 jioni katika eneo la Butuja A Kata ya Pasiansi wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza ambapo kichanga hicho kiliokotwa na wananchi katika ziwa Viktoria akiwa amefariki dunia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmedi Msangi ameeleza kuwa wananchi wametoa taarifa katika kituo cha polisi kuhusiana na tukio hilo ndipo walifika eneo la tukio na kufanya upelelezi na kufanikiwa kumkamata mwanamke huyo ambaye alikiri kuhusika na tukio hilo na kwamba Chanzo cha ukatili huo wa kutupa mtoto uliopelekea hadi kufariki dunia bado hakijafahamika .
Amesema kuwa Jeshi la Polisi lipo katika mahojiano na mtuhumiwa, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalo mkabili huku mwili wa kichanga hicho ukihifadhiwa katika Hospitali ya mkoa ya Sekou Toure kwa ajili ya uchunguzi na kwamba ukikamilika, mwili utakabidhiwa kwa ndugu na jamaa kwa ajili ya mazishi.
Msangi ametoa wito kwa wananch na wakazi wa jiji la Mwanza na kuwataka kuwa karibu na wamama wajawazito pindi wanapokuwa wanahitaji kusaidiwa ili kuweza kuepusha matatizo ambayo yanaweza kuepukika.
Alifafanua kwamba endapo ikibainika mtu anatenda tukio la aina hiyo kwa nia ya uovu, hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.