ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 2, 2017

MAMIA YA WAAFRIKA WATIWA MBARONI KATIKA MJI WA COLOGNE UJERUMANI.

Polisi ya Ujerumani imewatia nguvuni mamia ya watu wenye asili ya Afrika katika mji wa Cologne nchini humo.
Mamia ya watu hao wamekamatwa katika sehemu ya oparesheni ya polisi ya Ujerumani ya kuzuia kukaririwa mashambulizi ya kigaidi kama yale yaliyoikumba nchi hiyo mwaka uliopita wa 2016. Watu hao wamekamatwa katika vituo viwili vikuu vya treni ili kuhojiwa na kuchunguzwa utambulisho wao. 
Polisi ya mji wa Cologne imesambaza askari zaidi ya 1500 katika maeneo yote ya mji huo kwa ajili ya kudumisha usalama katika kipindi hiki cha sherehe za mwaka mpya. Sherehe za mwaka mpya wa 2017 zilimalizika nchini Ujerumani jana saa sita usiku huku ulinzi ukiwa umeimarishwa vikali.
Polisi wakiwa wamesambaza katika mji wa Berlin katika sherehe za mwaka mpya.
Sherehe za mwaka mpya zimefanyika nchini Ujerumani, huku nchi hiyo ikikumbuka tukio la kuuliwa watu 12 na kujeruhiwa wengine kadhaa baada ya mtu mmoja kuvurumisha lori katika soko la Krismasi katika mji wa Berlin tarehe 19 mwezi Disemba mwaka jana wakati watu wakifanya manunuzi.
Lori lililovurumishwa kwenye soko la Krismasi huko Berlin

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.