ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 10, 2017

WILAYA YA SENGEREMA YAPIGA MARUFUKU POMBE ZA KIENYEJI ZINAZOTENGENEZWA NA MAZAO YA CHAKULA.


NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza
KUFUATIA changamoto ya ukosefu wa chakula katika baadhi ya maeneo Mkoani Mwanz Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Emanuel Kipole amepiga marufuku utengenezaji wa Pombe za kienyeji kwa kutumia mazao ya chakula  badala yake wahifadhi mazao hayo ili yawasaidie hapo baadae.

Kipole ameeleza kuwa kumekuwa na changamoto ya ukame na pia  mazao kunyauka na kwamba hali hiyo inaweza kupelekea kuwepo kwa balaa la njaa katika baadhi ya maeneo huku akiwataka wananchi kutumia vizuri chakula walichonacho tofauti na wanavyo fanya sasa.

“Acheni kutumia chakula kutengenezea pombe, hali ya hewa mnaiona jinsi ilivyo, mvua hakuna mazao yanakauka na inasikitisha kuona baadhiyenu bado mnatumia hata akiba ya chakula mlichonacho kutengenezea pombe za kienyeji jambo ambalo ni hatari” alizema Kipole.

Mkuu huyo wa wilaya alitumia nafasi hiyo kuongea na wananchi wa kijiji cha Rubanda kata ya Kahumulo Wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Kampeni  wa Chama Cha Mapinduzi wilayani humo ambapo alieleza kuwa Serikali imeliona hilo kwamba itafanya kila jitihada katka kuhakikisha wananchi wanapata chakula nawanaishi katika hali ya usalama.

Wakizungumza na waandishi mara baada ya mkutano, baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wameeleza jinsi pombe hiyo inavyo tengenezwa kwa kutumia mazao ya chakula huku wakidai kuwa idadi kubwa ya wakazi hutumia njia hiyo ili kujipatia kipato.

Mmoja wa wananchi hao Bonifasi Ndege amesema  kuwa pombe hiyo inatengenezwa kwa kutumia mahindi ambapo hulowekwa kwa muda wa siku mbili, na kisha kuhifadhi katika mfuko mgumu ili yaweze kuoza, baada ya hapo hukaushwa na kupelekwa mashineni kwa ajili ya kusaga ili kutengenezea pombe na kwamba huenda hatua ya mwisho ikapatikana gongo kupitia uzalishji wake.

Hata hivyo Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza Antony Diallo amewatahadharisha wananchi hao na kuwataka kuhifadhi chakula kwa wingi, kwani makubaliano ya Serikali ni kupeleka chakula ambacho kitauzwa kwa Bei tofauti na iliyopo sokoni  kwa sasa na sio kugawa bure kama baadhi ya watu wanavyo dhani.

Ameeleza kuwa hii ni kutokana na kuwepo kwa ongezeko la bei za vyakula katka masoko mbalimbali nchini kutokaa a upungufu wa chakula huku akisisitiza wananchi kulima mazao yanayo vumilia ukame.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.