Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas amemwandikia barua Rais mteule wa Marekani Donald Trump na kumuonya juu ya taathira hasi za pendekezo lake la kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi Quds Tukufu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Palestina la WAFA, Abbas amemuonya Trump katika barua hiyo na kubainisha kuwa, kutekelezwa mpango huo kutakuwa ni kuhujumu uhuru wa taifa la Palestina na hivyo ajiandae kupambana na matokeo yake.
Kadhalika Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amewaandikia barua viongozi wa China, Russia na Umoja wa Ulaya akiwataka wafanye kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa azma hiyo ya Marekani haitekelezwi.Rais mteule wa Marekani Donald Trump. |
Akihutubia wananchi Ijumaa iliyopita katika mji wa Bait Laham (Bethlehem), Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Mahmoud Abbas alisema iwapo Marekani itatekeleza azma hiyo ya kubadilisha hali ya Quds Tukufu itakuwa imevuka mstari mwekundu, jambo ambalo Wapalestina hawatalikubali.
Kufuatia hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio dhidi ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina mwezi uliopita, Trump alisisitizia udharura wa ubalozi wa nchi hiyo ulioko Tel Aviv uhamishiwe haraka mji wa Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.