Taarifa kwa vyombo vya habari
Airtel yagawa faida ya shilingi milioni 3.5 kwa wateja wa Airtel Money
Dar es salaam, Kampuni ya simu za mkononi ya Airte leo imetangaza kuanza kwa mgawo wa faida yao wanaoipata kupitia huduma ya Airtel Money ambapo jumla ya shilingi bilioni 3.5 zaitagawiwa kwa wateja wake.
Faida ya Airtel Money inayogawiwa itawafaidisha wale wote wanaotumia huduma hiyo wakiwemo wateja, wachuuzi wadogo na wakubwa (wakala) kuanzia leo. Mgawo wa faida hiyo utategemea sana na salio la fedha ambalo mteja atakuwa amepitisha kwenye akaunti yake ya Airtel Money kwa kipindi cha robo ya mwaka.
Akiongelea kuhusu utaratibu wa ugawaji wa faida hiyo Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “ Hii ni mara ya nne toka Airtel Tanzania ilipoanza kulipa faida ya Airtel money kwa wateja wetu pamoja na wakala wote nchini, hadi sasa tokea kuanza kwa utaratibu huu kwa ujumla tayari tumeshagawa zaidi ya bilioni shilingi 11.8 TZS tokea tulivyoanza kufanya hivi mwezi Desemba mwaka 2015”.
Airtel tunajisikia fahari sana kutangazia uma wa watanzania leo hii kwamba wateja wetu kwa mwezi wa Junuari watapokea faida hii ili iwasaidie kufanya mambo mengi hasa tukiamini kuwa huu ni mwezi mgumu kama unavyotajwa na jamii. Dhamira yetu iko pale pale tunawapa wateja kila mmoja sawasawa na kiwango chake alichoweza kupitisha kwenye akaunti yake ya Airtel Money kisha ataitumia atakavyo kulingana na mahitaji yake”
“Huduma yetu ya Airtel Money imekuwa sana kutokana na wateja wetu kuitumia mara kwa mara. Airtel Money kwa sasa imefanikiwa kwa kufanya mihamala mingi katika na kusaidia maeneo mengi nchini ambayo hayajafikiwa na huduma za kibenki. Airtel tunachukua nafasi hii kuendelea kuwahamasisha wateja wetu wa Airtel Money kuendelea kuiamini huduma yetu na kuitumia kikamilifu katika mambo mbalimbali yanayohusiana na malipo ya pesa za kimtandao ili waendelee kujipataia faida kubwa wakati wa mgao wa faida tunayogawa kila ifikapo robo ya mwaka” alimaliza kusema Mmbando
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.