ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 28, 2016

UN KUSHIRIKI KATIKA UFUMBUZI WA MGOGORO WA BURUNDI.

Katibu Mkuu Mteule wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa umoja huo una irada thabitii ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa ndani nchini Burundi.

Antonio Guterres amemtumia ujumbe wa maandishi Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi na kubainisha kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kushiriki kwa dhati katika juhudi za kuupatia suluhisho mgogoro wa ndani wa Burundi. Antonio Guterres ataanza rasmi kazi kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi Januari mwakani. 
Katibu Mkuu Mteule wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa Burundi inakabiliwa na changamoto za pande kadhaa zilizosababishwa na mgogoro wa ndani na kwamba Umoja wa Mataifa utafanya kila linalowezekana ili kurejesha amani ya kudumu huko Burundi. Antonio Guterres hata hivyo amesema kuwa mchakato huo utategemea ushirikiano utakaotolewa na serikali ya Burundi.
Ghasia za mitaani zilizoigubika Burundi kufuatia hatua ya Rais Nkurunziza ya kugombea kiti cha rais kwa mara ya tatuAAA

ntonio Guterres pia ametoa mwito kwa Rais wa Burundi kutafuta njia pana ya kuiondoa nchi hiyo katika mkwamo wa kisiasa. Burundi ilitumbukia katika mzozo wa ndani mapema mwaka jana kufuatia hatua ya Rais Nkurunziza ya kutangaza azma yake ya kugombea kiti cha rais kwa mara ya tatu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.