ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 29, 2016

Sky News: MAELFU YA WATU NI WATUMWA MAMBOLEO NCHINI UINGEREZA.

Maandamano dhidi ya utumwa mamboleo Uingereza
Ripoti mpya inaonesha kuwa, karibu watu elfu 13 nchini Uingereza ni wahanga wa vitendo viovu vya kutumiwa kama watumwa wa ngono, kazi za kulazimishwa na aina nyingine za utumwa mamboleo.
Ripoti iliyotolewa na kituo cha Sky News cha Uingereza imesema kuwa, serikali ya nchi hiyo inafanya mikakati ya kutenga dola milioni 49 kwa shabaha ya kupambana na utumwa mamboleo nchini humo katika mwaka ujao wa 2017.
Ripoti hiyo imesema kuwa Shiika la Taifa Linaloshughulikia Uhalifu (NCA) limetangaza kuwa asilimia 25 ya wahanga wa utumwa mambo leo nchini humo ni watoto wadogo. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, maelfu ya wahanga na waathirika wa utumwa nchini Uingereza wanasumbuliwa na aina mbalimbali ya utumwa  mamboleo kama utumwa wa ngono na kazi za kulazimishwa.
Naibu Nkurugenzi wa Wakala wa Wahajiri nchini Uingereza, Andy Radcliffe amesema hivi karibuni polisi ya nchi hiyo imezitoza faini zaidi ya kampuni 60 kwa makosa ya kuwatumikisha wahamiaji kinyume cha sheria.
Jumuiya nyingi za kimataifa za kutetea haki za binadamu zimekuwa zikipaza sauti kulaani utuma na unyanyasaji mkubwa unaofanyika katika nchi zinazodai zimeendelea kama Uingereza dhidi ya wahamiaji na watu wa mataba ya chini. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.