ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 29, 2016

CHIDI BENZ: "NINAUMWA SANA NINAWEZA KUFA MUDA WOWOTE"

chidi-1-copy
Mtandao wa Global umeripoti habari waliyoifanyia uchunguzi na hadi kufanikiwa kumnasa Chid Benz Kwenye Chumba cha Hotel anayoishi...
Mtandao huo umeripoti hivi:

DAH, KUMBE CHID ANAUMWA HERNIA

Aliposogea, OFM lilimlaki kwa shangwe na kumchangamkia kiasi kilichomfanya atulie, akae chini na kuanza kupiga stori kwa zaidi ya saa moja, huku mara kwa mara akilalamika kuwa anaumwa sana ugonjwa wa Hernia na pia uvimbe chini ya kitovu ambao unamsababishia maumivu makali.  Chid alikuwa ameshika karatasi mkononi iliyoandikwa namba za simu za prodyuza Lamar ikadondoka chini, katika hali ya kushangaza alishindwa kuiokota maana kila alipoinama alihisi maumivu makali. OFM wakamsaidi a kuokota karatasi hiyo.
.
Chid: Washikaji msione nipo hivi lakini kiukweli ninaumwa sana, ninaweza kufa muda wowote, huu uvimbe chini ya kitovu unaniuma sana (akatoa wembe na kutaka kuuchana huo uvimbe, OFM mmoja alimdaka na kumsihi asifanye hivyo, akakubali baada ya kubembelezwa kwa muda).
.
OFM: Lakini kwa nini sasa unabwia unga na upo katika hali hii?

Chid: Uvimbe huu ndio unasababisha, nisipobwia unaniuma mno, sasa huwa nautuliza kwa kuvuta.

Baada ya maongezi ya muda mrefu, Chid aliwaamini wageni wake kiasi cha kuwakaribisha chumbani kwake, kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo. Chumbani, OFM walishangaa kumuona Chid akitoa mfuko chini ya godoro, ambao ndani yake kulikuwa na sigara, wembe, kipande cha kigae, mirija na kopo la soda lenye maji nusu, likiwa limetobolewa na mrija kupitishwa.

Baada ya kutoa vifaa hivyo, Chid alikaa na kutoa kete za madawa ya kulevya na kuanza kuandaa kwa ajili ya kubwia. Huku akichukuliwa picha za video kwa uhodari wa hali ya juu bila kufahamu, mara mbili alishtukia kuwa anarekodiwa.

Lakini hata hivyo, kila aliposhtuka, alipoozwa kwa maneno matamu ya stori zikaendelea hadi saa tisa usiku.

OFM: Sasa Chid kwa nini hutaki kuachana na haya madawa wakati watu mbalimbali wanajaribu kukusaidia?

CHID: Aaah, nishawaambia ninaumwa, hata watu wanaonisaidia wamekwisha niambia niendelee tu kutumia taratibu lakini nijali uhai nisizidishe nisije kufa.
GPL.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.