ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 17, 2016

HUKUMU DHIDI YA KESI YA BULAYA KESHO.

      Stephen Wasira                                                                           Ester Bulaya
Mwanza. Hatima kesi ya ubunge ya Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya na aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015 Stephen Wasira itajulikana kesho wakati Jaji Noel Chocha atakapotoa hukumu.

Awali, hukumu ya shauri hilo namba 01/2015 lililofunguliwa na wapigakura wanne ilipangwa kutolewa Novemba 22, lakini Jaji Chocha amerudisha nyuma kwa siku nne hadi kesho.

Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Francis Kabwe alithibitisha jana kuwa badala ya Novemba 22, sasa hukumu itatolewa kesho.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.