ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 25, 2016

CDEA WAZINDUA MRADI WA ATAMISHI YA KAZI ZA SANAA ‘IIDEA’ KUSAIDIA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

dsc_1296
Afisa wa Mradi wa IIDEA, Bi. Angela Kilusungu wa CDEA, akisoma taarifa fupi juu ya mradi huo mpya wa utakaosaidia sanaa kwa Afrika Mashariki
dsc_1316
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya CDEA, wakiwa katika mkutano huo
dsc_1354
Msanii Remigius Sostenes wa CDEA akitoa burudani katika tukio hilo





dsc_1337
Mwenyekiti wa Bodi wa CDEA, Mzee Madaraka Nyerere akijadiliana jambo na Mjumbe wa bodi hiyo ambaye anatokea Burundi, Bw. Gilbert Hagabimana wakati wa uzinduzo huo.
dsc_1357
Msanii Nick wa Pili akielezea namna sanaa inavyohitaji ubunifu wakati wa tukio hilo
dsc_1406
Wadau wa sanaa wakifuatilia makala fupi ya CDEA iliyokuwa maalum wakati wa uzinduzi huo



dsc_1427
Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa akielezea jambo katika tukio hilo
dsc_1440
Mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa Bw.Habibu Msammy aliyemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizindua rasmi mradi huo






dsc_1434
Mzee Kitime mmoja wa wadau wa Sanaa nchini akifuatilia kwa makini tukio hilo la uzinduzi
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Culture and Development East Africa (CDEA) leo limezindua rasmi mradi wa Atamishi ya kazi za sanaa (IIDEA) ambapo utakuwa nguzo muhimu kwa nchi za Umoja Wa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa Bw.Habibu Msammy aliyemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye, ameeleza kuwa sanaa ni ajira hivyo mpango huo utasaidia kuinua ajira kwa wasanii watakaofikiwa na kukuza soko la Afrika Mashariki kupitia Sanaa zao.

dsc_1438
Wadau wa kifuatilia uzinduzi huo
“Sanaa ni kazi ya kujikimu na kazi ni hutu hivyo ni wajibu wa kila msanii kujiheshimu na kufuata taratibu ili kuwa njia kwa jamii na kuheshimika zaidi hasa katika sanaa yake. Nawapongeza sana CDEA kwa mpango huu kwani utaendelea kudumisha umoja wa Afrika Mashariki, utasaidia Wasanii wetu kupanua mawazo yao zaidi na kujiongezea maarifa ya juu katika taaluma yao ya Sanaa.” Alieleza Bw. Habibu Msammy.

dsc_1471
Pia alisisitiza kuwa mafunzo watakayoyapata wayatumie kujiimalisha kiuchumi huku akisisitiza kuwa bado wanayo nafasi ya kujifunza zaidi katika kuweza kubuni vazi la Taifa.
“Kwa kuwa mradi huu unagusa sanaa za Ubunifu wa mavazi, Urembo na filamu. Wabunifu wa Tanzania ni wasaha wa kuendelea kubuni vazi la Taifa, Wasanii wanaangaliwa na wengi hivyo kuanzia mavazi na mawazo yao ya ubunifu na tunawategemea pia katika kubuni vazi letu la Taifa” alieleza Habibu Msammy.
cdea
Wajumbe wa Bodi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya uzinduzi wa mradi huo wa IIDEA, mapema leo Novemba 25.2016.
PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE.
Mradi huo wa mwaka mmoja unatarajia kuanza kutoa mafunzo kwa wabunifu wa mavazi na urembo, Wanamuziki na wasanii wa filamu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa amebainisha kuwa, baada ya mwezi mmoja kuanzia sasa wataanza mchakato wa kupata washiriki ambapo wahusika watatakiwa kutuma maombi ya ushiriki baada ya kuona matangazo mbalimbali yatakayotolewa na CDEA kupitia mitandao ya kijamii na sehemu zingine za Utamaduni.
Katika uzinduzi huo, watu mbalimbali wameshiriki wakiwemo wasanii wa filamu, maigizo, wabunifu wa mavazi, wanahabari, wanamuziki na wasanii wa kazi za sanaa ikiwemo za mikono na ubunifu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.