Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiendesha kidampa, huku msafara wa viongozi walioongozana naye akiwemo Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ukimfuatilia ni jana wakati alipotembelea uwanja mkongwe wa Nyamagana Jijini Mwanza, ili kujionea zoezi la uwekaji wa nyasi bandia kwenye uwanja huo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameeleza kuridhishwa na uwekaji wa nyasi bandia kwenye uwanja huo ambapo amewashukuru wadau wote waliofanikisha ukarabati wake wakiwemo wajasiriamali Jijini Mwanza ambao kodi zao zimesaidia upatikanaji wa zaidi ya shilingi Milioni 190 kutoka Halmashauri ya Jiji hilo ambazo zilizojumuishwa na dola za Kimarekani Laki Tano zilizotolewa na Shirikisho la Soka Duniani FIFA kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Altaf Hiran Mansoor ambaye ni mdau wa michezo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, amesema kampuni hiyo iko tayari kuchangia ukarabati wa uwanja huo ikiwemo ujenzi wa majukwaa.
|
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.