Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi na afya serikali kuu (TUGHE) Mkoa wa Pwani akizungumza na katika mafali ya shule hiyo ya wanafunzi wa darasa la saba. |
SHULE ya msingi lulanzi iliyopo kata ya picha ya ndege Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani bado inakabiliwa na changamoto ya pungufu wa nyumba vya madarasa,nyumba za walimu na ofisi,matundu ya vyoo,miundombinu mibovu, pamoja na uhaba wa madawati hivyo kusababisha wanafunzi hao kusoma katika mazingira magumu na hatarishi kwa upande wao.
Hayo yamebainishwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Laurencia Mallya wakati wa sherehe za mahafali ya 11 ya kuhitimu wanafunzi wa darasa la saba yaliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo,ambapo amesema kunahitajika juhudi za makusudi kutoka serikalini na kwa wadau wa maendeleo ili kuweza kuzitatua changamoto zinazowakabili na kuunga juhudi za serikali katika kuboresha sekta elimu.
Mmoja wa wahitimu hao Ally Kombo akisoma lisala kwa niaba ya wanafunzi wenzake wameiomba serikali ya awamu ya tano kuwaangalia kwa jicho la tatu kwa kuwatafutia fursa za kujiendeleza zaidi pindi wanapokosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza lengo ikiwa kuweza kujiajiri wao wenyewe na kujitegemea ili kuondokana na janga la umasikini wanalokabiliana nalo.
Naye mmoja wa wakinamama Suzan John akizungumza kwa niaba ya wazazi na walezi wenzake amewaasa wanafunzi hao kuepukana na tabia ya kuiga na kutojiingiza kabisa katika makundi ya vijiweni ambayo muda mwingi yanajihusiha na uvutaji wa madawa ya kulevya pamoja na kushiriki katika uharifu wa kupora mali za watu kitu ambacho ni kinyume cha sheria za nchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi na afya serikali kuu
(TUGHE) Mkoa wa Pwani ambaye alikuwa mgeni rasmi Catherine Katele amechangia kiasi cha laki tano na kuwataka walimu kuachana na vitendo vya ukatili kwa wanafunzi kwa kuwapa adhabu kali ya vipigo kinyume kabisa na sheria zilizowekwa na nchi hivyo wanapaswa kubadilika na kujikita zaidi katika suala la maadili na ufundishaji ili kuongeza kasi ya kiwango cha ufaulu.
Alisema kuwa anasikitishwa sana na kuona baadhi ya walimu wamekuwa hawana huruma hata kidogo kwa kuamua kuwaadhibu wanafunzi kitu ambacho ni kinyume kabisa na haki za binadamu na kuomba serikali kuwachukulia hatua kali kwa wale wote watakaobainika wanahusika katika matukio mbali mbali ya kikatili.
“Mimi tukio la kule mbeya kwa wale walimu ambao walikuwa wamekwenda kufanya kazi kwa vitendo lakini hii sio sahii kabisa hata kidogo kwani mwanafunzi anapaswa kupewa adhabu kulingana na kosa lake lakini sio kumpa kipigo kama sio binadamu, kwa hii walimu nawaomba kubadilika ili kuweza kuhakikisha wanawafundisha watoto ili waweze kufaulu,”alisema Catherine.
KATIKA mahafali hayo mgeni rasmi aliweza kuendesha zoezi la kushitukiza la kufanya harambee kwa wazazi pamoja na wanachi waliohudhuria ambapo alifanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni tatu na nusu kwa ajili ya kuweza kusaidia ujenzi wa vyoo,madarasa pamoja na nyumba ya mwalimu katika shule hiyo ya msingi lulanzi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.