Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Bw. Erest Makale akitoa taarifa hii leo katika ofisi zake. |
Kwa mujibu wa Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ernest Makale anasema kuwa Bi. Felister Mathias Mawe aliomba shilingi 500,000/= kutoka kwa mwananchi huyo ili aweze kumsaidia kupata nafasi ya kujiunga na jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)
BOFYA KUSIKIA TAARIFA HIYO.
Mtuhumiwa Bi. Felister Mathias Mawe akisimulia waandishi wa habari kilichotokea mpaka akaingia kwenye mtego huo wa kutapeli. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA. |
Mtuhumiwa Bi. Felister Mathias Mawe |
Mwanajeshi Mstaafu Bi. Sophia Chacha. |
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Bi. Felister alikamatwa na TAKUKURU mnamo tarehe 10/10/2016 katika Hoteli ya Wendele iliyopo Kirumba jijini Mwanza.
Mtuhumiwa tajwa amekuwa akijipatia fedha kwa watu mbalimbali waliokuwa wakihitaji kujiunga na jeshi hilo kwa madai kwamba atawasaidia kupta nafasi kwa kiwango cha shilingi laki tano (500,000/=) kwa kil mmoja.
Aidha kwa mujibu wa ushahidi uliopatikana kitendo cha mtuhumiwa kujifanya Afisa wa Jeshi hakihusiani na Makosa yaliyo chini ya sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Namba 11/2007, hivyo jalada lenye tuhuma hiyo namba PCCB/MZ/ENQ/40/2016 limehamishiwa kwa Wakili wa Seriali Mfawidhi ili Mtuhumiwa aweze kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Vipi hali ya Rushwa kwa mkoa wa Mwanza, na Sekta, Vitengo vipi vimekithiri kwa Rushwa? Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ernest Makale anafunguka zaidi.....BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.